Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 82

An-Nahl 16:82

النحل

فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ

Maana

Kwa hivyo, wakikengeuka, basi lililo juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wakikengeuka lilio juu yako wewe ni kufikisha ujumbe waziwazi. [82]

[82] Wakikupuuza, ewe Nabii, hao unao waita wafuate Uislamu, basi wewe huna jukumu kwa mapuuza yao. Haikulazimu wewe ila kufikisha ujumbe kwa uwazi, na hayo umekwisha fanya.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakikupa mgongo, ewe Mtume, baada ya kuziona hizi aya, basi usisikitike. Kwani jukumu lako ni kuufikisha ujumbe uliotumwa nao waziwazi, ama kuongoa ni kwetu sisi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net