An-Nahl 16:83
النحليَعْرِفُونَ نِعْمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ
Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni makafiri. [83]
[83] Kupuuza kwao hao makafiri si kwa kuwa hawajui kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu ndiye chanzo cha kila neema zote wanazo zipata, lakini wao hutenda vitendo vya wanao kanya neema, kwa vile hawamshukuru Mola Mlezi kwazo. Na wengi wao wamekazania kuwafuata baba zao katika kumkataa Mwenyezi Mungu, mpaka wakawa wengi wao ndio wapinzani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Washirikina hawa wanazijua neema za Allah Mtukufu juu yao za kutumwa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwao, kisha wanaukanusha utume wake. Na wengi wa watu wake ni wale wanaoukanusha utume wake na sio wanaoukubali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net