Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Sura ya 16

An-Nahl

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 76

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَآ أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَىٰهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِى هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ 76

{76} Nao mfano wa pili ni mfano wa, "Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote" si kichache wala kingi, "naye ni mzigo kwa mlezi wake" yaani, mlezi wake anahudumia naye hawezi hata akajihudumia mwenyewe. Kwa hivyo, ana mapungufu kwa kila njia. Basi je, yuko sawa huyu na yule, "anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka?" Kwani, maneno yake ni ya uadilifu, na matendo yake yamenyooka. Kwa hivyo, kama vile hawawi sawa, basi hawi sawa yeyote mwenye kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, ambaye hana uwezo wa chochote cha masilahi yake. Kwani kama si Mwenyezi Mungu kumfanyia hivyo, asingeweza kufanya chochote katika hayo. Hivyo basi, hawezi kufanana, wala kuwa mwenza wa yule ambaye hasemi isipokuwa haki, na wala hafanyi isipokuwa yale anayosifiwa juu yake.