An-Nahl 16:71
النحلوَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِى ٱلرِّزْقِ ۚ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُوا۟ بِرَآدِّى رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَآءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ
Na Mwenyezi Mungu amewaboresha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walioboreshwa hawarudishi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale ilio wamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu? [71]
[71] Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kwa riziki kuliko wengineo. Amemruzuku bwana mwenye kumiliki kuliko mtumwa mamluki. Wala walio ruzukiwa kingi hawawapi watumwa wao hata nusu ya riziki yao, ili wapate kuwa wote na riziki sawa! Basi ikiwa hawa makafiri hawakubali watumwa wao washirikiane nao katika riziki iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu, nao wote ni wanaadamu kama wao, basi vipi wao wanataka kumshirikisha Mwenyezi Mungu na viumbe vyake katika mambo yasio kuwa laiki naye Subhanahu wa Taa'la, nako ni kustahiki kuabudiwa? Basi je, macho ya hao washirikina yataendelea kufumbika baada ya yote haya, wakabaki wakipinga neema za Mwenyezi Mungu juu yao kwa kumshirikisha Yeye na wengineo?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewafanya bora baadhi yenu kuliko wengine katika riziki Aliyowapa ulimwenguni: katika nyinyi kuna tajiri na katika nyinyi kuna masikini, katika nyinyi kuna anayemiliki na katika nyinyi kuna anayemilikiwa, wenye kumiliki hawawapi wenye kuwamiliki kile Alichowapa Allah Mtukufu cha kuwafanya wawe na kiwango cha mali sawa na wao. Basi iwapo hawaliridhii hilo kwenye nafsi zao, ni kwa nini wanaridhika kumfanya Allah Mtukufu kuwa ana washirika miongoni mwa watumwa Wake? Kwa kweli huu ni udhalimu mkubwa kabisa na ukanushaji mkubwa kabisa wa neema za Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net