An-Nahl 16:2
النحليُنَزِّلُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦٓ أَنْ أَنذِرُوٓا۟ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ
Huwateremsha Malaika na ufunuo kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake kwamba onyeni kuwa hakuna mungu yeyote isipokuwa Mimi, basi nicheni Mimi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huwateremsha Malaika na Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake ili nyinyi muonye kwamba hapana mungu ila Mimi, basi nicheni Mimi. [2]
[2] Mwenyezi Mungu huteremsha Malaika kwa yanayo huisha nyoyo katika Wahyi wake (ndio hiyo Roho) juu ya anaye mkhiari kumpa Utume katika waja wake, ili watu wajue kwamba hapana mungu wa kuabudiwa kwa Haki ila Mimi. Basi jitengeni na yanayo nikasirisha na yatayo kuleteeni adhabu. Na shikamaneni na ut'iifu ili ukukingeni na adhabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Anawateremsha Malaika kuleta wahyi kwa amri Yake kwa anayemtaka miongoni mwa waja Wake waliotumilizwa kwamba waonyeni watu na ushirikina na waambieni kwamba hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi. Hivyo basi, nicheni kwa kutekeleza faradhi zangu na kunipwekesha kwa kuniabudu na kunitakasa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net