Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 3

An-Nahl 16:3

النحل

خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۚ تَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Maana

Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na wanayo shirikisha. [3]

[3] Yeye ameumba mbingu na ardhi kwa mujibu wa hikima. Ametakasika kuwa na mshirika wa kufanya lolote katika utawala wake, au wa kuabudiwa kama Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, ili waja kwa hizo wachukue ushahidi juu ya utukufu wa Muumba wa hizo na kwamba, Yeye Peke Yake, Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, na Ametukuka na ushirikina wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net