Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 4

An-Nahl 16:4

النحل

خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ

Maana

Amemuumba mtu kwa tone la manii. Na tazama, akawa mshindani aliye dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri. [4]

[4] Amemuumba kila mmoja katika wanaadamu kutokana na maji maji yasiyo shikamana, nayo ni manii. Kutokana na hayo ndio anakuwa mtu mwenye nguvu za kujitetea nafsi yake, mshindani na makhasimu zake, mwenye kuweka wazi hoja zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Amemuumba binadamu kutokana na maji dhalili, akitahamaki ajiona ana nguvu na majivuno, na akawa mkali wa utesi na kumjadili Mola wake katika kukanusha kufufuliwa na mengineyo, kama vile kusema, «Ni nani atakayeihuisha mifupa iwapo itaoza.» Na akawa ni mwenye kumsahau Allah Mtukufu Aliyemuumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net