An-Nahl 16:5
النحلوَٱلْأَنْعَـٰمَ خَلَقَهَا ۗ لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَـٰفِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ
Na aliwaumba wanyama. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya kutia joto,na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. [5]
[5] Enyi waja! Mwenyezi Mungu amekufadhilini - amekuumbieni nyama hoa, wanyama wa kufuga, kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, ili mpate kutokana na sufi zao na manyoa yao vifaa vya kukupatieni joto kujihifadhi na baridi, na mle nyama yao mhifadhi uhai wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanyama miongoni mwa ngamia, ng’ombe na mbuzi, Allah Mtukufu Amewaumbia, enyi watu, na akajaalia joto katika sufi na manyoya yake, na manufaa mengine katika maziwa yake na ngozi zake na kuwatumia kwa kuwapanda na, wengine miongoni mwao, kuwala.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net