Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 6

An-Nahl 16:6

النحل

وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ

Maana

Na katika hao mnapata furaha pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na mnapo wapeleka malishoni asubuhi. [6]

[6] Na mnapata kwao raha na furaha mnapo waona wanarejea kutoka machungani na matumbo yao na viwele vimejaa, na mnapo toka nao kwenda makondeni na machungani wakikimbilia malisha yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na muna, kwa wanyama hao, pambo linaloingiza furaha kwenu, pindi mnapowarudisha kwenye mazizi yao jioni na pindi mnapowatoa kukicha kuwapeleka malishoni.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net