An-Nahl 16:7
النحلوَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا۟ بَـٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلْأَنفُسِ ۚ إِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Nao hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyo weza kuifikia ila kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole na Mwenye kurehemu. [7]
[7] Na wanakubebeeni mizigo yenu mizito mpaka kwenye miji ambayo hamwezi kuifikilia bila yao isipo kuwa mzitie nafsi zenu katika juhudi na mashaka makubwa. Hakika Mola wenu Mlezi aliye kutengenezeeni hayo yote kwa ajili ya raha yenu bila ya shaka ni Mwingi wa upole, na Mkunjufu wa rehema kwenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanabeba wanyama hawa vyombo vyenu vizito kuvipeleka kwenye mji wa mbali ambao hamkuwa ni wenye kuufikia isipokuwa kwa usumbufu mwingi wa nafsi zenu na mashaka makubwa. Hakika Mola wenu ni Mpole, Mwenye huruma kwenu kwa kuwafanyia vitu mnavyovitaka kuwa ni vyepesi. Hivyo basi kusifiwa ni Kwake na kushukuriwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net