Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 8

An-Nahl 16:8

النحل

وَٱلْخَيْلَ وَٱلْبِغَالَ وَٱلْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Na farasi, nyumbu, na punda ili muwapande, na wawe ni pambo. Na anaumba msivyovijua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na farasi, na nyumbu, na punda ili muwapande, na kuwa ni pambo.Na ataumba msivyo vijua. [8]

[8] Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni farasi, na nyumbu, na punda mpate kuwapanda. Na mnawafanya ni pambo la kuingiza furaha katika nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu atakuja umba msivyo vijua sasa, katika vyombo vya kupanda na vya kukata masafa miongoni mwa alivyo msahilishia Mwenyezi Mungu binaadamu pindi akitumia akili yake na akafikiri kwayo, na akaongoka kwa kutumia kila uwezo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Amewaumbia farasi, nyumbu na punda, mpate kuwapanda na wawe ni pambo kwenu nyinyi na maangalizi mazuri. Na Anawaumbia nyinyi aina mbalimbali za vipando na vinginevyo ambavyo nyinyi hamna ujuzi navyo, ili mzidi kumuamini na kumshukuru.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net