Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 9

An-Nahl 16:9

النحل

وَعَلَى ٱللَّهِ قَصْدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنْهَا جَآئِرٌ ۚ وَلَوْ شَآءَ لَهَدَىٰكُمْ أَجْمَعِينَ

Maana

Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia. Na zipo njia za upotovu. Na angelipenda, angeliwaongoa nyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia. Na zipo njia za upotovu.Na angeli penda angeli kuongoeni nyote. [9]

[9] Na juu ya Mwenyezi Mungu, kwa mujibu wa fadhila yake na rehema yake, kukuonesheni Njia Iliyo Nyooka ya kukufikisheni kwenye kheri. Na zipo njia zilizo potoka zisio fika kwenye Haki. Na lau angeli taka kukuongoeni nyote angeli kuongoeni kwenye Njia Iliyo Nyooka, lakini amekuumbieni akili ya kutambua, na matakwa ya kuelekea, na akakuacheni na khiari yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ni juu ya Allah Mtukufu kuwaeleza njia iliyonyooka ya kuwaongoa nyinyi, nayo ni Uislamu. Na miongoni mwa njia kuna iliyoenda kombo isiyofikisha kwenye uongofu, nayo ni kila njia iliyo kinyume na Uislamu miongoni mwa mila na itikadi. Na lau Angalitaka Allah Mtukufu kuwaongoza, basi Angaliwaongoza nyote kwenye Imani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net