An-Nahl 16:10
النحلهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً ۖ لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ
Yeye ndiye anayewateremshia maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye anaye kuteremshieni maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia. [10]
[10] Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka jiha ya mbinguni. Katika hayo mnapata kunywa, na mengine ndio inapelekea miti kumea. Nanyi hupeleka wanyama wenu wakale kwenye miti hiyo, nao wakupeni maziwa, na nyama, na sufi, na manyoa, na nywele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye Ndiye Aliyewateremshia mvua kutoka juu na Akawapatia nyinyi kwa hiyo mvua maji mnayokunywa na akawatolea kwa maji hayo miti ya nyinyi kuwalisha wanyama wenu, na yanarudi kwenu matumizi yake na manufaa yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net