Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 11

An-Nahl 16:11

النحل

يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرْعَ وَٱلزَّيْتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلْأَعْنَـٰبَ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Maana

Kwa hayo Yeye anawaoteshea mimea, na mizaituni, na mitende, na mizabibu, na kila aina ya matunda. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaotafakari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hayo Yeye anaizalisha kwa ajili yenu mimea, na mizaituni,na mitende, na mizabibu, na kila namna ya matunda. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao fikiri. [11]

[11] Kwa maji yateremkayo mbinguni humea makulima ambayo tunakutoleeni nafaka na mizaituni, na mitende, na mizabibu na mengineyo, katika kila namna ya matunda mlayo mbali yaliyo tajwa. Hakika kuwepo vitu hivi ni alama ya kuwaongoa watu wanao nufaika kwa akili zao, wakazingatia uwezo uliyo patisha hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Anawatolea nyinyi kutoka kwenye ardhi, kwa maji haya, mazao mbalimbali: Anawatolea nyinyi kwayo mizaituni, mitende na mizabibu, na anawatolea nyinyi kwayo kila aina ya matunda, makubwa kwa madogo. Hakika katika hayo pana ushahidi wa wazi kwa watu wanaofikiri na wakazingatia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net