An-Nahl 16:12
النحلوَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ ۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتٌۢ بِأَمْرِهِۦٓ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
Na amewatiishia usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zimetiishwa kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kaumu watumiao akili.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi,na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili. [12]
[12] Na Mwenyezi Mungu ameufanya usiku ukutumikieni kwa kuufanya uwe ndio wakati wenu wa kupumzika na mchana ni muwafaka kuhangaika kwenu na kwenda kwa kazi zenu, na jua kukuleteeni joto na mwangaza, na mwezi mpate kujua idadi ya miaka na hisabu, na nyota zinazo kutumikieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu ili mpate kujua njia katika kiza. Hakika katika hayo zipo alama na dalili kwa watu ambao wananufaika kwa akili aliyo wapa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Amewadhalilishia usiku kwa mapumziko yenu, na mchana kwa maisha yenu, na Amewadhalilishia jua likawa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na ili mpate kujua miaka na hesabu na manufaa mengine yasiyokuwa hayo. Na nyota huko mbinguni zimedhalilishwa kwa ajili yenu kwa amri ya Allah Mtukufu, ili mjue nyakati, kuiva kwa matunda na mazao na pia kuongoka kwa nyota hizo kwenye giza. Hakika, katika kudhalilisha huko, kuna alama za wazi kwa watu wanaotia mambo akilini mwao kuhusu Allah Mtukufu, hoja Zake na alama Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net