An-Nahl 16:13
النحلوَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَٰنُهُۥٓ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ
Na vile alivyowaenezea katika ardhi vya rangi mbalimbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaokumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hivi alivyo vieneza katika ardhi vya rangi mbali mbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa watu wanao waidhika. [13]
[13] Na pamoja na aliyo kuumbieni Mwenyezi Mungu katika mbingu na akakutengenezeeni kwa faida yenu, amekuumbieni pia juu ya ardhi wanyama namna nyingi, na mimea, na vitu visio na uhai. Na ndani ya ardhi yamo maadeni ya rangi na sura mbali mbali na faida mbali mbali. Na yote hayo kwa manufaa yenu. Hakika katika hayo zipo dalili wazi na nyingi kwa watu wanao zingatia, na wakawaidhika, na wakajua kwa hayo uwezo wa Aliye waumba, na rehema yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Amewadhalilishia vile Alivyowaumbia katika ardhi miongoni mwa vinavyotambaa humo na matunda na madini na visivyokuwa hivyo ambavyo vina rangi na manufaa mbalimbali. Hakika katika uumbaji huo na kutafautiana rangi na manufaa pana mazingatio kwa watu wanaowaidhika na wanaojua kwamba katika kuvidhalilisha vitu hivi pana alama nyingi juu ya umoja wa Allah Mtukufu Aliyetukuka na juu ya kumpwekesha kwa ibada.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net