Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 14

An-Nahl 16:14

النحل

وَهُوَ ٱلَّذِى سَخَّرَ ٱلْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا۟ مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُوا۟ مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى ٱلْفُلْكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Maana

Yeye ndiye aliyeitiisha bahari, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa. Na utaona merikebu zikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayo yavaa. Na unaona marikebu zikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru. [14]

[14] Ni Yeye aliye idhalilisha bahari, na akaifanya ikutumikieni, mpate kuvua na mle nyama za samaki, laini na mpya mpya. Na mtoe humo baharini mapambo kama lulu na marijani. Na ewe mwenye kuangalia ukazingatia, unaona marikebu zinavyo pita baharini zikikata maji nazo zimesheheni bidhaa na vyakula. Mwenyezi Mungu ameyadhalilisha hayo ili mnafuike nyinyi, na mtafute riziki kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa njia ya biashara na nyenginezo, na mpate kumshukuru kwa aliyo kutengenezeeni, na hayo ni kwa kukutumikieni nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye Ndiye Ambaye Amewadhalilishia bahari ili mpate kula nyama laini ya samaki mnaowavua, na mtoe humo pambo mnalolivaa kama lulu na marjani, na utaziona jahazi kubwa zinapasua uso wa maji zikienda na kurudi, na mnazipanda ili mtafute riziki ya Allah Mtukufu kwa kufanya biashara na kutafuta faida ndani yake. ili mumshukuru Allah Mtukufu Aliyetukuka kwa neema zake kubwa juu yenu na msimuabudu asiyekuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net