An-Nahl 16:15
النحلوَأَلْقَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَـٰرًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
Na akaweka katika ardhi milima madhubuti ili ardhi isiyumbeyumbe nanyi. Na mito, na njia mbalimbali ili mpate kuongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kaweka katika ardhi milima ili ardhi isiyumbe yumbe nanyi.Na mito, na njia ili mpate kuongoka. [15]
[15] Na Mwenyezi Mungu amefanya katika ardhi milima iliyo simama imara, ili kuizuia isiyumbe yumbe.(Mwaka 1956 wataalamu wa geology, ilimu ya tabaka za ardhi, wamegundua kuwa kweli milima inasaidia kuizuia ardhi isitaharaki na kuachana. Wamevumbua kuwa mabara, continents, yamo katika kutaharaki. Kwa mfano kusini ya Amerika iliambatana na Afrika ya Magharibi, na ilisota mpaka ikafanyikana milima ya Andes. Hali kadhaalika Milima ya Himalaya ikazuia kusota kwa Bara Hindi. Pia wamegundua kuwa maki ya gamba la ardhi kwa kawaida halizidi kilomita 6, lakini chini ya milima hufika hata kilomita 35. Basi ni kweli kuwa milima ni kama vigingi vya kuzuia ardhi isiyumbe, kama ilivyo sema Qur'ani miaka 1400 iliyo pita.) Na Mwenyezi Mungu amefanya katika ardhi mito inayo pita na maji yanayo faa kunywa na kunyweshea makulima, na njia zilizo tengenezwa ili mpate kuzipitia kwendea mtakako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Ameyakitisha kwenye ardhi majabali ya kuithibitisha ili isije ikawayumbisha nyinyi, na Ameiweka humo mito ili mpate kunywa maji yake, na Amefanya humo njia nyingi ili mpate kuongoka kwa njia hizo kuzifikia sehemu mnazozikusudia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net