An-Nahl
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَٱلْخَيْلَ وَٱلْبِغَالَ وَٱلْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ 8
{8} "Na farasi, nyumbu, na punda" mara mnawatumia katika kuwapanda kwa lazima na mara kwa ajili ya kutafuta uzuri na pambo, na hakutaja kuwala hawa, kwa sababu ni haramu kumla nyumbu na punda, na pia mara nyingi farasi hawaliwi, bali inakatazwa kuwachinja kwa ajili ya kuwala kwa kuhofia waje kukosekana. Vinginevyo, imethibiti katika Kitabu cha hadithi Sahihi kwamba Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliruhusu kula nyama ya farasi. "Na anaumba msivyovijua" katika vile vitakavyokuwa baada ya kuteremka kwa Qur-ani miongoni mwa vitu ambavyo viumbe wanavipanda katika nchi kavu, baharini, hewani, na wanavitumia katika faida zao na masilahi yao. Hivyo hakuvitaja kwa majina yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutaja katika Kitabu chake isipokuwa kile ambacho waja wake wanakijua au wanajua kinachofanana nacho. Na ama kile kisichokuwa na mfano wake, basi lau hicho kingetajwa, basi hawangekijua wala hawangefahamu makusudio yake. Ndiyo maana akataja msingi unaokusanya yale wanayoyajua na wasiyoyajua, kama alivyotaja neema za Peponi, na akataja humo kile tunachokijua na tunatazama mfano wake, kama vile mitende, mizabibu, makomamasi, na akataja kwa ujumla yale tusiyoyajua katika kauli yake "Humo katika kila matunda zimo namna mbili." Basi vile vile hapa ametaja kile vile tunavyovijua miongoni mwa vipando, kama vile farasi, nyumbu, punda, ngamia, safina, na akajumuisha vinginevyo katika kauli yake, "Na anaumba msivyovijua."