An-Nahl 16:1
النحلأَتَىٰٓ أَمْرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiiharakishe. Ametakasika na ametukuka mbali na hayo wanayomshirikisha nayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiihimize. Ametakasika na Ametukuka na wanayo mshirikisha nayo. [1]
[1] Enyi washirikina! Kuweni na yakini kwamba aliyo kuahidini Mwenyezi Mungu kuwa yatakuwa Siku ya Kiyama yapo karibu kutokea bila ya shaka. Basi msifanye maskhara kwa kuyahimiza yatokee. Mwenyezi Mungu ametakasika na kuwa na mshirika wa kuabudiwa badala yake. Na hiyo miungu mnayo mshirikisha naye haiwezi jambo lolote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kumekaribia kusimama Kiyama na kutoka amri ya Allah Mtukufu ya kuwaadhibu nyinyi, enyi makafiri, basi msiifanyie haraka adhabu kwa njia ya kuicheza shere ahadi ya Mtume kwenu. Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Ametakasika na ushirika na washirikina.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net