Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.

Hadithi 18

Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera

عَنِ العَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، عَلِّمْنِي شَيْئًا أَسْأَلُهُ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ. قَالَ: «سَلِ اللَّهَ العَافِيَةَ»، فَمَكَثْتُ أَيَّامًا ثُمَّ جِئْتُ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، عَلِّمْنِي شَيْئًا أَسْأَلُهُ اللَّهَ. فَقَالَ لِي: «يَا عَبَّاسُ، يَا عَمَّ رَسُولِ اللهِ، سَلِ اللَّهَ العَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ».
Kutoka kwa Al-Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu nitakachomuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu. Akasema: "Muombe Allah afya", nikakaa siku kadhaa kisha nikarudi, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nifundishe kitu ambacho nitamuomba Mwenyezi Mungu. Akasema kuniambia: "Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaNi sahihi kwa sababu ya hadithi nyinginezo
Maelezo

Ami yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake Al-Abbas bin Abdul Muttalib Allah amuwie radhi alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamfundisha amuombe Mwenyezi Mungu afya njema na salama kutokana na balaa na kasoro za Dini, Dunia na Akhera, akasema: Baada ya siku chache nikarejea kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa mara nyingine tena nikimuomba anifundishe dua nimuombe Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake akimwambia kwa mapenzi na upole: Ewe Abbas, ewe ami wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya aondoe madhara yote na alete kheri na manufaa katika Dunia na Akhera.

Mafunzo
  1. Kurudiarudia kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake jibu hilo hilo kwa Abbasi alipomuuliza kwa mara ya pili kunaonyesha afya ndio jambo la heri zaidi mja analomuomba Mola wake Mlezi.
  2. Kumebainishwa fadhila za afya nakuwa imekusanya heri zote katika Dunia na Akhera.
  3. Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kutaka kuongeza elimu na heri.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 491) (3514). مسند أحمد (3/ 303) (1783). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (2/ 1014). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 468). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 566). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص815). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 40).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهما أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ: «اللهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ، وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ، وَبِكَ خَاصَمْتُ، اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ أَنْ تُضِلَّنِي، أَنْتَ الْحَيُّ الَّذِي لَا يَمُوتُ، وَالْجِنُّ وَالْإِنْسُ يَمُوتُونَ».
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".
Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim, na matamshi haya ni ya Muslim, na akaipokea Bukhari kwa ufupiDarajaSahihi
Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimejisalimisha" na nimenyenyekea, "na kwako nimeamini" na nimesadikisha na nimekiri, "Na juu yako nimetegemea" na nimekabidhi na nimetegemea, "na kwako nimetubia" na nimerejea na nimekuja, "na kwako ninapambana" na ninajibizana kwa hoja na maadui zako, "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako" Ninajiegemeza, "kwa utukufu wako" na ngome yako na ushindi wako, "hapana mola wa haki isipokuwa wewe" na wala hakuna muabudiwa wa haki zaidi yako, "unipoteze" kutoka katika uongofu na taufiki ya kupata radhi zako, "Wewe ndiye uliye hai ambaye hafi" na wala hamaliziki, "na majini na watu wote wanakufa".

Mafunzo
  1. Sheria ya kutanguliza sifa katika kila mahitaji.
  2. Ulazima wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na kuomba hifadhi kutoka kwake; kwa sababu yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa kamilifu, basi yeye peke yake yake ndiye mwenye kutegemewa, na viumbe wote hawajiwezi na mwisho wao ni kifo, hivyo wao hawastahiki kutegemewa.
  3. Kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua kwa maneno haya yaliyokusanya kila kitu, na yenye kuzuia kingenecho kuingia humo, yanayoelezea kwa imani ya kweli na yakini ya kiwango cha juu.
  4. Amesema As-Sa'diy: Kauli yake: "Wewe ndiye uliye hai" Yaani: Wewe pekee ndiye unayestahiki kuombwa kinga na si mwingine zaidi yako.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 117) (7383). صحيح مسلم (4/ 2086) (2717). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص72). فتح رب البرية بتلخيص الحموية، لابن عثيمين (ص79). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 109). مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، عبيد الله المباركفوري (8/ 223).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ: «يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، آمَنَّا بِكَ وَبِمَا جِئْتَ بِهِ فَهَلْ تَخَافُ عَلَيْنَا؟ قَالَ: «نَعَمْ، إِنَّ القُلُوبَ بَيْنَ أُصْبُعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ اللهِ يُقَلِّبُهَا كَيْفَ يَشَاءُ».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upotofu. Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake alistaajabu kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiiomba dua hii mara kwa mara, basi Mtume rehema na amani zimshukie akamwambia kuwa nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, huzigeuza apendavyo, hivyo, moyo ni kituo cha imani na ukafiri, na moyo umeitwa Qalbu kwa sababu ya kugeukageuka kwake mara kwa mara, moyo hugeuka sana kuliko chungu kinapokusanyika kile kinachotokota ndani yake. Amtakaye Mwenyezi Mungu huudumisha moyo wake katika uongofu na uthabiti katika Dini, na anayemtaka Mwenyezi Mungu huugeuza moyo wake kutoka katika uongofu na kuupeleka katika upotofu.

Mafunzo
  1. Kujisalimisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na kunyenyekea kwake, na kuuelekeza umma kuliomba hilo.
  2. Umuhimu wa kuwa na msimamo na uthabiti katika dini, na kuwa kinachozingatiwa ni hatima ya mtu ya maisha yake.
  3. Mja hawezi kujitosheleza mwenyewe hata kwa kupepesa jicho bila ya kutiwa uthabiti na Mwenyezi Mungu katika Uislamu.
  4. Himizo la kuomba dua hii kwa wingi, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  5. Kudumu katika Uislamu ni neema kubwa ambayo mja anatakiwa kuifanyia juhudi na kumshukuru Mola wake Mlezi.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 19) (2140). مسند أحمد (19/ 160) (12107). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 476). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 567). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1014). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص808). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 41).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: «اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْهُدَى وَالتُّقَى، وَالْعَفَافَ وَالْغِنَى».
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.

Mafunzo
  1. Utukufu wa mambo haya: Uongofu, uchamungu, na kujizuia na machafu, na kutosheka, na himizo la kujipamba nayo.
  2. Mtume rehema na amani ziwe juu yake hamiliki juu ya nafsi yake manufaa wala madhara, na kwamba anayemiliki hayo ni Allah Mtukufu.
  3. Anayemiliki manufaa na madhara na uongofu kwa viumbe ni Mwenyezi Mungu peke yake, si Malaika aliyekaribu wala Mtume aliyetumwa wala yeyote asiyekuwa wao.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2087) (2721). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 146). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص68). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 183). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 528). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 104).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya

عَن قُطْبَةَ بنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الأَخْلاَقِ وَالأَعْمَالِ وَالأَهْوَاءِ».
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga" Yani: Ninaomba ulinzi na ukaribu "kwako" na si kwa asiyekuwa wewe, "kutokana tabia mbovu" alizozikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "katika tabia" kama chuki na husuda na kiburi, "na" mabaya "katika matendo" kama kutukana na kushutumu, "na" yote "matamanio", ambayo nafsi inayatamani hali yakuwa yanakwenda kinyume na sheria.

Mafunzo
  1. Ubora wa dua hii na kujibiwa kwake.
  2. Muumini anapupia kuepuka tabia mbaya na matendo maovu, na anachukua tahadhari ya kufuata matamanio na kutumbukia katika matamanio.
  3. Kugawanyika kwa tabia na matendo na matamanio katika maovu na mazuri.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 544) (3591). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 389). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 248). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (7/ 436).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «اللهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي الَّتِي فِيهَا مَعَادِي، وَاجْعَلِ الْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْرٍ، وَاجْعَلِ الْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa dua iliyokusanya ndani yake misingi ya tabia njema alizotumwa kuzitimiliza; nazo ni kutengenezewa dini, na dunia, na Akhera, akachota kutoka katika matamshi haya mafupi kutengemaa kwa mambo makubwa matatu, na akaanza na kutengemaa kwa dini, ambayo ndiyo sababu ya kutengemaa hali ya Dunia na Akhera, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu" Kwa kuniafikisha kusimamia adabu zake kwa namna iliyokamilika na kutimia zaidi. "Ambayo ndiyo ngome ya jambo langu" Na iwe hifadhi kwa mambo yangu yote, ikiwa dini yangu itaharibika basi yataharibika mambo yangu, na nitapata hasara na kutoka patupu, na kwakuwa hakuwezi kutimia kutengemaa kwa dini inayotakiwa isipokuwa kwa kutengemaa dunia, akasema: "Na unitengenezee dunia yangu" Kwa kunipa afya ya mwili na amani, na riziki, na mke mwema, na kizazi kizuri na yale ninayoyahitaji, na yawe ya halali, na yanisaidie katika kukutii, kisha akataja udhuru katika kuomba kwake kutengemaa kwake; kwa kusema: "Ambayo kuna maisha yangu" Na mahala pa kuishi kwangu na muda wa uhai wangu. "Na unitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu" Na kurejea kwangu ili kukutana na wewe, na hii ni kwa kutengemaa kwa matendo, na Mwenyezi Mungu kumuwezesha mja katika ibada na ikhlasi, na kuupata mwisho mwema. Na akapangilia rehema na amani ziwe juu yake Akhera baada ya dunia; kwa sababu ya kwanza ndio sababu ya kutengemaa ya pili, atakayekuwa na msimamo katika dini yake kwa namna atakavyo Mwenyezi Mungu, basi Akhera yake itanyooka na atapata furaha ndani yake. "Na uufanye uhai" Yaani: Na kurefushwa kwa umri "Kuwa ni ziada kwangu katika kila kheri" Ili nizidishe amali njema, "Na uyafanye mauti" na kuharakishwa kwake "Raha kwangu kutokana na kila shari" Na fitina na mitihani na majaribu kwa maasi na kughafilika, na ili iwe ni sababu ya kuepukana na matatizo ya Dunia na shida zake, na kupatikana kwa raha.

Mafunzo
  1. Dini ndio kitu muhimu; na ndio maana alianza nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua.
  2. Dini ndio ngao ya mwanadam inayomkinga dhidi ya kila shari.
  3. Kuomba mambo ya kidunia kwa ajili ya kutengeneza dini na Akhera.
  4. Si vibaya kutamani kufa kwa kuhofia mitihani na fitina katika dini, au kumuomba Mwenyezi Mungu kufa katika shahada.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2087) (2720). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 581). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 471). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 512). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (2/ 715).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza

عَنِ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ كَانَ يَدْعُو بِهَذَا الدُّعَاءِ: «رَبِّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي وَجَهْلِي، وَإِسْرَافِي فِي أَمْرِي كُلِّهِ، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطَايَايَ، وَعَمْدِي وَجَهْلِي وَهَزْلِي، وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أَخَّرْتُ، وَمَا أَسْرَرْتُ وَمَا أَعْلَنْتُ، أَنْتَ المُقَدِّمُ وَأَنْتَ المُؤَخِّرُ، وَأَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ».
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akiomba kwa dua hii: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilizokusanya mambo mengi ni kauli yake: "Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe makosa yangu" "na dhambi zangu", na yale yaliyotokea kwangu pasina kujua. "Na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote" na uzembe wangu na kuvuka kwangu mipaka. "Na yale uyajuayo kutoka kwangu" Uliyoyajua ewe Mwenyezi Mungu lakini mimi nimeyasahau. "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe makosa yangu na makusudi yangu" Na yale yaliyotokea kwa makusudi na kwa kujua kwangu kuwa ni dhambi. "Na niliyodhamiria na yale ya mzaha" Na yale yaliyotekea kwa mzaha, na yale yaliyotokea katika hali zote mbili. "Na hayo yote toka kwangu" Kiasi kwamba yote yaliyotajwa yamekusanya madhambi na aibu zote. "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza" Katika yale yaliyopita, "Na yale niliyoyachelewesha" Katika yale yatakayokuja. "Na yale niliyoyafanya kwa siri" niliyoyaficha "Na niliyoyatangaza" Na kuyaonyesha wazi. "Wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji" Unamtanguliza umtakaye katika viumbe wako katika rehema zako kwa kumpa taufiki katika yale unayoyaridhia, na wewe ndiye unayemchelewesha umtakaye katika hilo, kwa kumnyima uwezo, hakuna wa kuyapeleka mbele uliyoyachelewesha, na wala hakuna kuyachelewesha mambo uliyoyawahisha. "Na wewe juu ya kila kitu ni muweza" Yaani: Unauwezo uliokamilika na maamuzi timamu, mfanyaji pasina kizuizi cha yote uyatakayo.

Mafunzo
  1. Fadhila za dua hii, na kuipupia kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Katazo la kufanya ubadhirifu nakuwa mbadhirifu amejiingiza katika adhabu.
  3. Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua mwanadam vizuri zaidi kuliko anavyojijua, hivyo anatakiwa akabidhi mambo yake kwa Mwenyezi Mungu; kwani yeye anaweza kukosea pasina kujua.
  4. Mwanadam anaweza kuchukuliwa hatua kwa sababu ya mzaha wake kama anavyochukuliwa katika kukusudia kwake, hivyo ni wajibu kwa mwanadam achukue tahadhari katika mzaha wake.
  5. Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Sijaona chochote katika njia za mapokezi ya hadithi hii kuwa dua hii inasomwa mahala fulani, na riwaya zimekuja nyingi zikionyesha mwisho wake... kama kusema ndani ya swala za usiku, na riwaya za mapokezi zimetofautiana, je alikuwa akiisoma kabla ya salaam au baada yake? Na zote mbili zimeelezwa.
  6. Je, Mtume rehema na amani ziwe juu yake anakosea na kuomba msamaha? Imesemekana kuwa alisema hivyo kwa unyenyekevu na kwa kuitenza nguvu nafsi yake, na akachukulia kuwa kupitwa na ukamilifu na kuacha kilicho bora ni dhambi, au alikusudia yale yanayotokea kwa kusahau, au yale yaliyotokea kabla ya utume, na imesemwa kuwa: Kutaka msamaha ni ibada hivyo ni lazima kuileta, si kwa sababu ya kutaka kusamehewa pekee, bali ni kwa kumuabu Mwenyezi Mungu, na imesemwa kuwa: Hili ni angalizo na ni funzo kwa umma wake; ili wasijiaminishe na wakaacha kuomba msamaha.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 84) (6398). صحيح مسلم (4/ 2087) (2719). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 467). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 507). مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (5/ 1720).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera

عَنِ ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَعُ هَؤُلَاءِ الدَّعَوَاتِ، حِينَ يُمْسِي وَحِينَ يُصْبِحُ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي دِينِي وَدُنْيَايَ وَأَهْلِي وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَتِي -أَو: عَوْرَاتِي- وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي، وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي».
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".
Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha maombi haya pindi anaposhinda jioni na pindi anapoamka. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba afya" na kusalimika na magonjwa na mabalaa na shida za dunia, na matamanio na fitina za kidunia "Katika dunia na Akhera" kwa au kwa baadae "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha" na kusalimika na aibu, "Katika dini yangu" kutokana na ushirikina na uzushi na maasi, "na dunia yangu" katika majanga na kero na shari, "na familia yangu" mke wangu na wanangu na ndugu zangu, "na mali yangu" na mali zangu na matendo yangu. "Ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu" Yaani: Na yale yaliyokwangu katika aibu na dosari na mapungufu na ufute dhambi zangu, "na utie amani hofu yangu" Mfadhaiko wangu na hofu yangu. "Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi" Na uzuie kwangu balaa miongoni mwa yale yenye kuudhi na mabalaa, "mbele yangu na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu" Kiasi kwamba aliomuomba Mwenyezi Mungu amuhifadhi kutoka pande zote; kwa sababu mabalaa na maafa humfika mtu na kumuelekea kutoka moja kati ya pande hizi. "Na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa" na nisichukuliwe hatua toka chini yangu ghafla, nikaangamia ghafla "kutoka chini yangu" nikaangamia kwa kudidimizwa.

Mafunzo
  1. Kudumu na maneno haya kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Mwanadam kama alivyo anaamrishwa kumuomba Mwenyezi Mungu afya katika dini, vile vile kaamrishwa kumuomba katika dunia.
  3. Amesema Attwayibi: Imekusanya pande zote sita; kwa sababu maafa mengi hutokea katika pande hizo, na akatia mkazo katika upande wa chini kwa sababu maafa ya kutoka chini huwa mabaya zaidi.
  4. Kilicho bora wakati wa kusoma Adhkari, wakati wa asubuhi: Ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na kuanzia baada ya Lasiri mpaka kabla ya Maghribi, ikiwa atasema baada ya wakati huo, yaani: Akazisoma asubuhi baada ya Jua kunyanyuka itafaa pia, na hata akisema baaada ya Adhudhuri itamfaa pia, na ikiwa atazazisema baada ya Maghrib itamtosheleza pia, huo ndio wakati wa kufanya dhikri.
  5. Dalili ikionyesha kuwa dhikri inamuda maalum wakati wa usiku kama kusoma aya mbili za mwisho katika suratul baqara basi hii inakuwa ni baada ya kuzama kwa Jua.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 408) (5074). سنن النسائي (8/ 282) (5529). سنن ابن ماجه (5/ 37) (3871). مسند أحمد (8/ 403) (4785). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 565). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 441). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 491). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (2/ 711).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 18
Hadithi 18
  1. Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera
  2. Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa
  3. Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”
  4. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka
  5. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya
  6. Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu
  7. Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza
  8. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera
  9. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa
  10. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako
  11. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui
  12. Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto
  13. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa
  14. Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe
  15. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale
  16. Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima
  17. Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako
  18. Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com