Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba yeye alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba uongofu" na njia iliyonyooka katika kuijua haki na kuifanyia kazi, "na uchamungu", kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo, "na kujizuia na machafu" kujizuia na yale yasiyokuwa halali wala si mazuri miongoni mwa kauli au kitendo, "na kutosheka" na viumbe, kiasi ambacho asimuhitaji yeyote zaidi ya Mola wake Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.
Mafunzo
Utukufu wa mambo haya: Uongofu, uchamungu, na kujizuia na machafu, na kutosheka, na himizo la kujipamba nayo.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake hamiliki juu ya nafsi yake manufaa wala madhara, na kwamba anayemiliki hayo ni Allah Mtukufu.
Anayemiliki manufaa na madhara na uongofu kwa viumbe ni Mwenyezi Mungu peke yake, si Malaika aliyekaribu wala Mtume aliyetumwa wala yeyote asiyekuwa wao.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2087) (2721).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 146).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص68).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 183).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 528).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 104).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com