Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ أَكْثَرُ دُعَاءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اللَّهُمَّ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً، وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha dua kwa dua fupi zenye kukusanya mambo mengi, na miongoni mwake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Tupe hapa katika Dunia (mambo) mazuri, na Akhera utupe mazuri na utukinge na adhabu ya moto", Dua hii inakusanya mazuri yote ya Dunia; ikiwemo riziki ya raha na pana na ya halali, na mke mwema, na mtoto kitulizo cha jicho, na starehe, na elimu yenye manufaa, na mfano wa hayo miongoni mwa maombi yanayopendeka na ya halali, na mazuri ya Akhera ni kusalimika na adhabu za kaburi, na kisimamo cha Kiyama na moto, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu, na kufaulu kwa kupata neema za kudumu, na kuwekwa karibu na Mola Mlezi Mwingi wa huruma.

Mafunzo
  1. Sunna ya kuomba dua kupitia dua zinazokusanya maana pana, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Kwa ukamilifu zaidi ni mtu akusanye katika maombi yake baina ya kheri za Dunia na Akhera.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 83) (6389). صحيح مسلم (4/ 2070) (2690). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 578). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 463). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 504). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 714).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com