Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَدْعُو بِهَؤُلَاءِ الْكَلِمَاتِ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ، وَشَمَاتَةِ الْأَعْدَاءِ».
Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"
Imepokelewa na Nasai na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na mambo haya: La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda" na ninajikabidhi na kujiweka "kwako" si kwa mwingine, "kutokana na kuelemewa na deni" na kunitenza nguvu na misukosuko yake, na ninakuomba msaada wa kulilipa na kulitimiza. La pili: "Na kuzidiwa na adui" na kunitenza nguvu na kunitawala kimabavu, na ninakuomba uzuie adha zake, na unipe ushindi juu yake. La tatu: "Na kutukanwa na maadui" na kufurahi kwao kwa yale yanayowafika waislamu miongoni mwa mabalaa na misiba.

Mafunzo
  1. Himizo la kutaka ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na yote yanayomshughulisha mtu na ibada na kuleta msongo wa mawazo kama madeni na mengineyo.
  2. Deni la kawaida halina tatizo, isipokuwa tatizo ni kwa yule asiyekuwa na mali ya kulipa deni, na hili ndio deni linaloelemea.
  3. Mwanadam anatakiwa ayaepuke mambo yanayopelekea kutukanwa au kuabishwa kwayo.
  4. Kumebainishwa uadui wa makafiri kwa waumini na kufurahishwa kwao pale wanapofikwa na majanga.
  5. Maadui kudhihirisha furaha yao kwa mtihani wa mtu hili humuongezea maumivu makubwa kuliko hata balaa lenyewe.
Marejeo

سنن النسائي (8/ 265) (5475). مسند أحمد (11/ 189) (6618). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 569). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 450). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 497).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com