Kutoka kwa Abuu Said Al-Khudri amesema: Muawia alitoka kwenda msikitini akakuta kundi, akasema: Nini kimewakalisha hapa? Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema: Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililowakalisha isipokuwa hilo? Wakasema: Wallahi hakuna lililotukalisha isipokuwa hilo. Akasema: Basi tambueni kuwa sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu kwa lolote, na hakuna aliyekuwa katika nafasi yangu kwakuwa na mazungumzo machache zaidi kuliko mimi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: Na hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka kwenda katika kundi la Maswahaba zake na kusema: “Mbona mmekaa pamoja?” Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa kuwa ametuongoza kwenye Uislamu, na kwa kutujaalia. Akasema: “Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililokukalisheni isipokuwa hilo?" Wakasema: "Wallahi hatukukaa kwa lolote ila hilo.” Akasema: «Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alitoka Muawia bin Abi Sufian, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwenda katika kundi moja msikitini na akawauliza wamekusanyika kwa jambo gani, Wakasema: Tunamtaja Mwenyezi Mungu, basi akawaapisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba hawakutaka katika kikao chao na mkusanyiko wao isipokuwa ni kumtaja Mwenyezi Mungu, wakaapa kwa hilo, kisha akawaambia: Sikukuapisheni kwa tuhuma yoyote juu yenu au kuwa na shaka juu ya ukweli wenu, kisha akaeleza kuhusu hali yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba hakuna aliyekuwa karibu naye kuliko yeye. Kwa sababu Ummu Habiba alikuwa ni dada yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa wahyi, lakini ilikuwa ni nadra sana kusimulia hadithi, Basi akawaambia kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka nyumbani kwake na akawakuta wamekaa msikitini wakimdhukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa yale aliyowaongoza katika Uislamu na kuwakirimia. Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akawauliza na kuwaapisha sawa na alivyofanya Muawia kwa jamaa zake, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaambia kuhusu sababu ya kuwauliza kwake na kuapa kwao: kwamba Malaika Jibril, amani iwe juu yake, alimjia na kumwambia kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifakhirisha kupitia nyinyi kwa Malaika, na anawadhihirishia ubora wenu na anawaonyesha uzuri wa amali yenu, na anakusifieni mbele yao.
Mafunzo
Fadhila za Muawia, Mungu amuwie radhi, na pupa yake ya kumuiga Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika kufikisha elimu.
Inafaa kumwapiza mtu hata kama humtuhumu, bali kwa ajili tu kumzindua juu ya umuhimu wa kheri unayotaka kumueleza.
Fadhila za vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu, na vikao vya kielimu, nakuwa Mwenyezi Mungu huvipenda na hujifaharisha kwavyo mbele za Malaika.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2075) (2701).
نزهة المتقين (2/ 993).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 522).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 271).
Kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Je, nisiwaambieni matendo bora zaidi kwenu, na masafi zaidi mbele ya Mfalme wenu, na yatakayo kunyanyueni juu zaidi katika daraja zenu, na bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na pesa, na bora kwenu kuliko hata kukutana na adui yenu na mkapiga shingo zao na wakapiga shingo zenu?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: “Ni kumtaja Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
Hivi je mnata nikuelezeni na nikufundisheni amali bora zaidi kuliko zote katika amali zenu, na yenye utukufu kuliko zote na yenye kukua zaidi na safi zaidi na takatifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mfalme Aliyetukuka?
na yenye nafasi ya juu zaidi katika nafasi zenu za peponi?
na ambayo ni bora zaidi kwenu kuliko kutoa sadaka ya Dhahabu na fedha?
na bora kwenu kuliko hata kukutana na makafiri vitani, mkapiga shingo zao, na wakapiga shingo zenu?
Maswahaba wakasema: Ndio tunalitaka hilo.
Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni kumtaja Mwenyezi Mungu katika nyakati zote na katika mikao yote na hali zote.
Mafunzo
Nikuwa kudumu katika kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wazi na kwa siri ni katika mambo makubwa yanayomuweka mtu karibu na Mola wake, na yenye manufaa makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Vitendo vyote viliwekwa ili kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na simamisha sala kwa kunikumbuka". Naye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, amesema: "Kuizunguka Al-Kaaba na baina ya Safa na Marwah na kurusha mawe kulikusudiwa tu kumtaja Mwenyezi Mungu" Imepokelewa na Abu Daudi na Tirmidhiy.
Al-Izzi bin Abdul Salam amesema katika Qawaid yake: Hadithi hii inaashiria kwamba malipo hayatokani na kiwango cha uchovu katika ibada zote, bali Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweza kulipa zaidi kwa matendo madogo kuliko mengi, hivyo malipo yanatokana na tofauti za daraja katika utukufu.
Al-Munawiy amesema katika Faidh al-Qadir: Hadithi hii inafasiriwa kuwa dhikri imekuwa bora kwa wale walioambiwa kuifanya, kwakuwa, na lau kama mtu shupavu na shujaa angeliambiwa kuifanya na yakapatikana manufaa katika Uislamu basi ingeitwa Jihadi, au tajiri ambaye mali yake inawanufaisha masikini, basi ingeitwa sadaka, au mtu mwenye uwezo wa kuhiji, basi ingeitwa Hija, au mtu mwenye wazazi wawili, basi ingeitwa wema kwa wazazi, na kupitia kwake inapatikana taufiki kati ya habari na habari.
Dhikiri iliyokamilika zaidi ni ile ambayo ulimi umetamka ikiwa pamoja na mazingatio ya moyo, kisha ile iliyomo moyoni peke yake kama tafakuri, kisha inayokuwa kwa ulimi peke yake, na kila moja ina ujira, In shaa Allah.
Muislamu kudumu na dhikiri zenye kuendana na hali mbali mbali kama asubuhi na jioni, na kuingia msikitini na nyumbani na chooni na wakati wa kutoka, na nyinginezo, hii inamfanya kuwa miongoni mwa wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 389) (3377).
سنن ابن ماجه (4/ 705) (3790).
مسند أحمد (36/ 33) (21702).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 513).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 985).
كنوز رياض الصالحين لمجموعة من الباحثين.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akitembea katika njia ya kuelekea Makka, akapita karibu na mlima Jumdan, akasema: “Tembeeni huu ni mlima Jumdan, Wamepata ushindi wenye kujitenga” Wakasema: Ni akina nani hao wenye kujitenga ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika Wanaume, na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika wanawake.”
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza nafasi ya wale wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na kwamba wao ni wa kipekee na wametangulia wengine katika kufikia daraja za juu katika Bustani za neema, na akawafananisha na mlima Jumdan ambao ni wa kipekee ukilinganisha na milima mingine.
Mafunzo
Inapendeza kufanya dhikiri kwa wingi, na kushughulishwa nayo, kwa sababu kutangulia huko Akhera kunapatikana kupitia vitendo vingi vya utii na ikhlasi katika ibada.
Kumtaja Mwenyezi Mungu kunaweza kuwa kwa ulimi tu, au kwa moyo tu, au kwa ulimi na moyo pamoja ambayo ni kiwango cha juu zaidi.
Miongoni mwa dhikiri ni nyiradi za kisheria ambazo zimewekewa mipaka, kama vile dhikiri za asubuhi na jioni, na za baada ya sala za faradhi, na nyinginezo.
Amesema Al-Nawawi: Tambua kuwa fadhila za dhikiri hazikomei katika kumtukuza Mwenyezi Mungu (Tasbiih), na tahalil (Laa ilaaha illa llaah), na kumsifu (Tahmiid), na takbir (Allahu Akbar) na mengineyo, bali kila mwenye kumtii Mwenyezi Mungu basi huyo anamdhukuru Mwenyezi Mungu.
Ameeleza Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa sababu kubwa za kupewa uimara (Thabati), akasema Mtukufu: "Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa." [Al-Anfaal:45].
Sababu ya kufananisha kati ya wanaomtaja Mwenyezi Mungu na Mlima Jumdan ni upekee wake na kujitenga kwake. Mlima Jumdan umejitenga na milima mingine, hivyo hata wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu wamejitenga pia, mwenye kujitenga ni yule ambaye moyo wake na ulimi wake viko peke yake kwa kumkumbuka Mola wake Mlezi, hata akiwa miongoni mwa watu, na anapata faraja kwa nyakati anazojitenga, na anapata upweke nyakati anazokuwa na watu wengi. Na inaweza kuwa sababu ya kufananishwa mfano huo ni kuwa dhikiri ndio sababu ya uthabiti katika dini kama vile milima ni sababu ya kuimarika kwa ardhi, au ni kwakuwa anakuwa yeye ndiye wa kwanza kupata amali njema duniani na Akhera, kwa sababu msafiri anayetoka Madina kwenda Makka alikuwa anapofika Jumdan, ni dalili ya kuwa kafika Makka, na mwenye kuufikia anakuwa ndiye wa kwanza, basi hivyo hivyo mwenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu yuko mbele ya wengine kwa kumkumbuka kwake Mwenyezi Mungu kwa wingi, na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2062) (2676).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 983).
تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان، لابن سعدي (ص665).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 510).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 516).
Kutoka kwa bin Mas'udi radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam, nakuwa imenyooka na kulingana sawa, nakuwa mimea yake: ni (kusema) Sub-haana llaah -Ametakasika Mwenyezi Mungu, Na Alhamdulillaah -Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Na Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Allaahu Akbar -Mwenyezi Mungu Mkubwa".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaNi Nzuri kwa Ushahidi wake mbalimbali
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa alikutana na Ibrahim mwandani amani iwe juu yake usiku aliposafirishwa kwenda mbinguni (Israa wal Miiraji), akasema kumwambia: Ewe Muhammadi: Wafikishie umma wako kutoka kwangu salamu, na ulijulishe kuwa Pepo ina udongo mzuri, ina maji matam yasiyokuwa na chumvi, na kuwa Pepo ni pana, ni tambarare haina miti, na kuipanda kwake ni kwa maneno mazuri, nayo ni mema yenye kubakia: Sub-haanallaah, Alhamdulillaah, wa Laa ilaaha illa llaah, wallaahu Akbaru, kila anapoyasema muislamu na kuyarudiarudia hupandia mmea Peponi.
Mafunzo
Himizo la kudumu na dhikiri ili kukithirisha mimea ya Pepo.
Fadhila za umma wa kiislamu; kiasi kwamba Ibrahim amani iwe juu yake aliutumia salam.
Himizo la Nabii Ibrahim amani iwe juu yake kwa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake la kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Attwayibi: Pepo ni uwanda (tambarare), kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa fadhila zake akaweka ndani yake miti na magorofa kulingana na matendo ya watendaji; kila mfanyaji atakuwa na nafasi maalum kwa sababu ya matendo yake, kisha Mwenyezi Mungu alipompa wepesi wa kufanya matendo aliyoumbiwa ili azipate thawabu hizo, akamfanye yeye kuwa ni kama mpandaji wa miti hiyo.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 455) (3462).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين لسليم الهلالي (2/ 512).
الكاشف عن حقائق السنن (شرح المشكاة)، للطيبي (6/ 1831).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 186).
مشكاة المصابيح، للتبريزي (2/ 716).
مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للمباركفوري (7/ 476).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 985).
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba hakuna kundi la watu watakaokaa katika kikao kisha wakanyanyuka katika kikao hicho haliyakuwa hawajamtaja Mwenyezi Mungu ndani yake isipokuwa watanyanyuka katika mfano wa mzoga wa punda katika kunuka na uchafu; na hii ni kwa sababu walishughulika na mazungumzo wakaacha kumtaja Mwenyezi Mungu, na kikao hicho kwao kitakuwa ni masikitiko siku ya Kiyama na ni mapungufu na majuto kwao.
Mafunzo
Yaliyotajwa katika kutahadharisha kughafilika na kumtaja Mwenyezi Mungu hayaishii katika kikao pekee, bali yanaenea mahala pengine, amesema Imam Nawawi: Ni machukizo kwa atakayekaa mahali aondoke kabla hajamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake.
Masikitiko yatakayotokea kwao siku ya Kiyama: Ima kwa kupitwa na malipo na thawabu kwa kutofaidika na wakati katika kumtii Mwenyezi Mungu, na ima kwa madhambi na adhabu kwa kuutumia wakati kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.
Tahadhari hii ni pale kujisahau kutakapokuwa ni kwa mambo ya halali, vipi kwa vikao vya haramu ambavyo ndani yake kuna utesi na usengenyaji na mengineyo?!.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 221) (4855).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 120).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 654).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye utajiri: Wanaswali kama tunavyoswali na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka katika mali yao ya akiba. Akasema: Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi yawezekanaje akidhi mmoja wetu matamanio yake kisha awe na malipo? Akasema: Mnasemaje ikiwa atakiweka katika haramu, je atakuwa na mzigo wa dhambi? basi ndivyo hivyo akikiweka katika halali atakuwa na malipo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Walilalamikia baadhi ya mafukara wa kiswahaba hali ya umasikini wao kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutotoa kwao sadaka kwa mali ili wapate malipo mengi kama walivyoyapata ndugu zao wenye mali nyingi na ili na wao wafanye kheri kama wao; kiasi ambacho wao wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka kwa mali yao ya ziada na sisi hatutoi! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaelekeza katika yale wanayoyaweza katika sadaka, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwani hakukujaalieni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza kuvitoa sadaka kwa ajili nafsi zenu?! Kwani kauli yenu: "Sub-haanallaah" Inakuwa kwenu na malipo ya sadaka, na vile vile kauli: "Allaahu Akbar" ni sadaka, na kauli: "Alhamdulillaah" ni sadaka, na kauli: Laa ilaaha illa llaah" ni sadaka, na kuamrisha mema" ni sadaka, na "kukataza maovu" ni sadaka, bali hata katika tendo la ndoa la mmoja wenu kwa mke wake ni sadaka. Wakashangaa, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi akidhi mmoja wenu matamanio yake na awe na malipo katika hilo?! Akasema: Hivi mwaonaje kama akiweka katika haramu kama zinaa au kinginecho, je, atakuwa na madhambi? Hivyo hivyo akiweka katika halali anakuwa na malipo.
Mafunzo
Kushindana kwa Maswahaba katika kufanya kheri, na pupa yao ya kupata malipo na fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kukithiri kwa njia za amali za kheri, nakuwa zinakusanya kila amali anayoifanya muislamu kwa nia njema na lengo zuri.
Urahisi wa Uislamu na wepesi wake, kila muislamu anapata anayoweza kuyafanya ili amtii Mwenyezi Mungu kwayo.
Amesema Nawawi: Na katika hili kuna dalili yakuwa mambo ya halali yanaweza kuwa ibada kwa nia ya kweli, tendo la ndoa linakuwa ibada atakaponuia kukidhi haki ya mke na kushiriki naye kwa wema ambao ameamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutafuta mtoto mwema, na kuilinda nafsi yake na nafsi ya mke wake na kujizuia wote wawili na kutazama haramu, au kuifikiria, au kutamani kufanya, au mengineyo katika malengo mazuri.
Amepiga mfano na kupima kwa akili; ili jambo liwe wazi na liingie vizuri ndani ya nafsi ya msikilizaji.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 697) (1006).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 201).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 161).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 31).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 150).
Kutoka kwa Abdallah bin Busri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sheria za Uislamu zimekuwa nyingi kwangu, hebu nieleze kitu ambacho nitashikamana nacho, akasema: "Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.
Mafunzo
Fadhila za kudumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu ni kufanya sababu za kupata malipo kuwa nyepesi.
Watu kuzidiana katika mafungu yao katika milango ya wema na kheri.
Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa ulimi, kwa kumsabihi na kumhimidi, na kukiri kuwa hapana mola muabudiwa wa haki ila yeye, na kumtukuza, na mengineyo pamoja na moyo kwenda sambamba na ulimi, hili linakaa nafasi ya ibada nyingi za sunna.
Kuchunga kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya muulizaji kwa kumjibu kila linalomfaa.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 388) (3375).
سنن ابن ماجه (4/ 707) (3793).
مسند أحمد (29/ 226) (17680).
جامع العلوم والحكم في شرح خمسين حديثا من جوامع الكلم، لابن رجب الحنبلي (2/ 510).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص104).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للنووي وابن رجب (ص154).
الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد، لعبد الله بن صالح المحسن (ص93).
Kutoka kwa Agharri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu kukithirisha kuomba toba na msamaha, na anajielezea mwenyewe kuwa yeye hutubia kwa Mwneyezi Mungu Mtukufu na kumuomba msamaha kwa siku zaidi ya mara mia moja, na haliyakuwa alikwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, na katika hilo kuna ukamilifu wa kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Mafunzo
Kila mmoja vyovyote itakavyokuwa nafasi yake na daraja lake katika imani, basi anahitaji kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kuikamilisha nafsi yake kwa toba, nakuwa kila mmoja hakosi mapungufu katika kutimiza haki za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: "Na tubieni kwa Mwenyezi Mungu nyote enyi waumini".
Toba ni kwa mambo yote, sawa sawa kwa kufanya maharamisho au madhambi au uzembe katika kutimiza wajibu.
Ikhlasi (kutakasa nia) katika toba ni sharti la kukubaliwa kwake, atakayeacha dhambi kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu huyo bado hajatubia.
Amesema Nawawi: Toba ina masharti matatu: Ajivue katika maasi, na ajute kwa kuyafanya, na atie dhamira ya kweli ya kutorudi katika maasi mfano wake kabisa, na ikiwa maasi yanahusiana na haki ya binadamu basi kuna sharti la nne, nalo: Kurudisha haki aliyodhulumu kwa mwenye nayo, na kujivua nayo.
Tahadhari: Kuomba msamaha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuna maana kuwa kuna madhambi aliyafanya, lakini ni kwa sababu ya ukamilifu wa utumwa wake na kufungamana kwake na kumtaja Aliyetakasika na kutukuka, na kuvuta kwake taswira ya utukufu wa haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upungufu wa mja kwa namna yoyote atakayofanya katika kushukuru neema zake, nayo inakuwa ni sehemu ya kuwawekea sheria umma wake baada yake, na hukumu zinginezo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2075) (2702).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 33).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 97).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 52).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com