Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata kama yatakuwa na wingi mfano wa povu la Bahari

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ، فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ، حُطَّتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayesema: Sub-haanallahi wabihamdihi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake) kwa siku mara mia moja (100), yatafutwa madhambi yake hata kama yatakuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayesema kwa siku mara mia moja (100): "Sub-haanallaahi Wabihamdihi"; Yatafutwa makosa yake na yatasamehewa, hata kama yatakuwa mengi mfano wa taka nyeupe (povu) zinazoelea Baharini wakati mawimbi yanapotembea na yanapopiga.

Mafunzo
  1. Malipo haya anayapata atakayelisema neno hilo ndani ya siku nzima mfululizo au kwa nyakati tofauti tofauti.
  2. Tasbihi: Ni kumtakasa Allah kutokana na mapungufu, na kumhimidi: Ni kumsifu kwa ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
  3. Makusudio katika hadithi hii ni kufutwa madhambi madogo madogo, ama madhambi makubwa haya ni lazima yafanyiwe toba.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 86) (6405). صحيح مسلم (4/ 2071) (2691). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 535). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 401). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 470). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 704).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Fadhila za Adh-kaar.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com