Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa alikutana na Ibrahim mwandani amani iwe juu yake usiku aliposafirishwa kwenda mbinguni (Israa wal Miiraji), akasema kumwambia: Ewe Muhammadi: Wafikishie umma wako kutoka kwangu salamu, na ulijulishe kuwa Pepo ina udongo mzuri, ina maji matam yasiyokuwa na chumvi, na kuwa Pepo ni pana, ni tambarare haina miti, na kuipanda kwake ni kwa maneno mazuri, nayo ni mema yenye kubakia: Sub-haanallaah, Alhamdulillaah, wa Laa ilaaha illa llaah, wallaahu Akbaru, kila anapoyasema muislamu na kuyarudiarudia hupandia mmea Peponi.
- Himizo la kudumu na dhikiri ili kukithirisha mimea ya Pepo.
- Fadhila za umma wa kiislamu; kiasi kwamba Ibrahim amani iwe juu yake aliutumia salam.
- Himizo la Nabii Ibrahim amani iwe juu yake kwa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake la kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Amesema Attwayibi: Pepo ni uwanda (tambarare), kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa fadhila zake akaweka ndani yake miti na magorofa kulingana na matendo ya watendaji; kila mfanyaji atakuwa na nafasi maalum kwa sababu ya matendo yake, kisha Mwenyezi Mungu alipompa wepesi wa kufanya matendo aliyoumbiwa ili azipate thawabu hizo, akamfanye yeye kuwa ni kama mpandaji wa miti hiyo.
سنن الترمذي (5/ 455) (3462). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين لسليم الهلالي (2/ 512). الكاشف عن حقائق السنن (شرح المشكاة)، للطيبي (6/ 1831). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 186). مشكاة المصابيح، للتبريزي (2/ 716). مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للمباركفوري (7/ 476). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 985).