Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Hapana Mola" na hakuna muabudiwa wa haki "isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika" katika uungu wake na ulezi wake na majina yake na sifa zake, "Ufalme ni wake" na maamuzi na mipangilio yote, "naye juu ya kila kitu ni muweza" pasina wa kumzuia wala wa kumkinga, na asiyoyataka hayawezi kuwa. Atakayesema dhikiri hii kwa siku mara mia moja, ataandikiwa ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu sawa na aliyeacha huru watumwa kumi, na ataandikiwa kwa maneno hayo mema mia moja na daraja Peponi, na yatafutwa kwake makosa mia moja, na yatakuwa ni kinga na kizuizi na ngome dhidi ya Shetani na upotovu wake na usaliti wake katika siku yake hiyo mpaka iingie jioni kwa kuzama jua, na hatoleta yeyote siku ya Kiyama kitu bora kuliko alichokuja nacho, isipokuwa mtu aliyefanya zaidi ya hivyo na akazidisha zaidi ya hapo.
- Ubora wa neno la Tauhidi na ukubwa wa malipo yake.
- Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kiasi ambacho kawawekea dhikiri nyepesi kwa kila mmoja, na akaipangia thawabu nyingi.
- Ikiwa atasema dhikiri hii (Tahalil) zaidi ya mara mia moja katika siku, basi atapata malipo yaliyotajwa katika hadithi ya mia moja, na atakuwa na thawabu nyingine za ziada, na hii si katika mipaka iliyozuiliwa kuivuka, na kupitiliza idadi yake, na kwamba kuzidisha kwake hakuna fadhila au kunaibatilisha.
- Amesema Nawawi: Dhahiri ya ujumla wa hadithi hii nikuwa anayapata malipo haya yaliyotajwa katika hadithi ni yule atakayesema tahlil hii (dhikiri) mara mia moja katika siku yake, sawa sawa awe aliyasema kwa mfululizo au tofauti tofauti katika vikao tofauti, au baadhi yake mwanzo wa mchana na mengine mwisho wake, lakini kilicho bora ayalete mfululizo mwanzo wa mchana, ili iwe ni kinga kwake katika mchana wake wote.
صحيح البخاري (4/ 126) (3293). صحيح مسلم (4/ 2071) (2691). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (5/ 300). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (42/ 136).