Kutoka kwa Abuu Said Al-Khudri amesema: Muawia alitoka kwenda msikitini akakuta kundi, akasema: Nini kimewakalisha hapa? Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema: Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililowakalisha isipokuwa hilo? Wakasema: Wallahi hakuna lililotukalisha isipokuwa hilo. Akasema: Basi tambueni kuwa sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu kwa lolote, na hakuna aliyekuwa katika nafasi yangu kwakuwa na mazungumzo machache zaidi kuliko mimi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: Na hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka kwenda katika kundi la Maswahaba zake na kusema: “Mbona mmekaa pamoja?” Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa kuwa ametuongoza kwenye Uislamu, na kwa kutujaalia. Akasema: “Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililokukalisheni isipokuwa hilo?" Wakasema: "Wallahi hatukukaa kwa lolote ila hilo.” Akasema: «Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alitoka Muawia bin Abi Sufian, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwenda katika kundi moja msikitini na akawauliza wamekusanyika kwa jambo gani, Wakasema: Tunamtaja Mwenyezi Mungu, basi akawaapisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba hawakutaka katika kikao chao na mkusanyiko wao isipokuwa ni kumtaja Mwenyezi Mungu, wakaapa kwa hilo, kisha akawaambia: Sikukuapisheni kwa tuhuma yoyote juu yenu au kuwa na shaka juu ya ukweli wenu, kisha akaeleza kuhusu hali yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba hakuna aliyekuwa karibu naye kuliko yeye. Kwa sababu Ummu Habiba alikuwa ni dada yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa wahyi, lakini ilikuwa ni nadra sana kusimulia hadithi, Basi akawaambia kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka nyumbani kwake na akawakuta wamekaa msikitini wakimdhukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa yale aliyowaongoza katika Uislamu na kuwakirimia. Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akawauliza na kuwaapisha sawa na alivyofanya Muawia kwa jamaa zake, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaambia kuhusu sababu ya kuwauliza kwake na kuapa kwao: kwamba Malaika Jibril, amani iwe juu yake, alimjia na kumwambia kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifakhirisha kupitia nyinyi kwa Malaika, na anawadhihirishia ubora wenu na anawaonyesha uzuri wa amali yenu, na anakusifieni mbele yao.
Mafunzo
Fadhila za Muawia, Mungu amuwie radhi, na pupa yake ya kumuiga Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika kufikisha elimu.
Inafaa kumwapiza mtu hata kama humtuhumu, bali kwa ajili tu kumzindua juu ya umuhimu wa kheri unayotaka kumueleza.
Fadhila za vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu, na vikao vya kielimu, nakuwa Mwenyezi Mungu huvipenda na hujifaharisha kwavyo mbele za Malaika.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2075) (2701).
نزهة المتقين (2/ 993).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 522).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 271).
عن أنس رضي الله عنه مرفوعاً: «من خَرج في طلب العلم فهو في سَبِيلِ الله حتى يرجع».
Kutoka kwa Anas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake hadithi Marfu'u: "Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri
Maelezo
Maana ya hadithi: Nikuwa atakayetoka nyumbani kwake au katika mji wake; kwaajili ya kutafuta elimu ya kisheria,huyo anakuwa katika hukumu ya aliyetoka kwaajili ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,mpaka atakaporudi kwa watu wake; kwasababu anakuwa ni kama mpiganaji katika kuihuisha kwake dini na kumdhalilisha shetani na kuitaabisha nafsi.
Mafunzo
Nikuwa kutafuta elimu ni kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Mwenye kutafuta elimu ana malipo ya mpiganaji katika viwanja vya mapambano; kwasababu wote hao wanayasimamia yale yanayoweza kuipa nguvu sheria ya Mwenyezi Mungu na wanazuia yasiyokuwa humo.
Ndani yake nikuwa mwenye kutoka katika kutafuta elimu atakuwa na malipo ya kutembea kwake na kwenda kwake na kurudi kwake mpaka atakaporejea kwa watu wake.
Marejeo
جامع الترمذي، تحقيق وتعليق:أحمد محمد شاكر وآخرون، مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي، ط2، مصر، 1395هـ.
دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، لمحمد علي بن محمد بن علان، ط4، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة، بيروت، 1425ه.
رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ.
رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ.
صحيح الترغيب والترهيب، للألباني، ط5، مكتبة المعارف – الرياض.
مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للمباركفوري، الطبعة الثالثة، إدارة البحوث العلمية والدعوة والإفتاء، الجامعة السلفية - بنارس الهند، 1404هـ.
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري، ط1، دار الفكر، بيروت، 1422هـ.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.
Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: "Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi, kukawa na kundi moja zuri lililokubali maji likaotesha malisho na majani mengi, na ilikuwa ni ardhi ni kame iliyomeza maji Mwenyezi Mungu akanufaisha watu kupitia ardhi hiyo wakanywa na wakanywesha na wakalima, na mvua hiyo ikashuka katika sehemu nyingine ya ardhi laini haitulizi maji na wala haioteshi mimea; Huu ndio mfano wa mtu aliyejifunza akaelimika katika dini ya Mwenyezi Mungu na yakamnufaisha aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu akajua na akafundisha, na mfano mwingine ni wa mtu ambaye hakuyatilia maanani na wala hakukubali uongofu wa Mwenyezi Mungu ambao nimetumwa nao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amefananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kumstaajabu yule anayenufaika na yale aliyokuja nayo miongoni mwa muongozo na njia inayomfikisha mtu katika lengo, na elimu ya kisheria na Ardhi ambayo inashukiwa na mvua nyingi; ikawa migawanyiko mitatu: Wa kwanza: Ardhi safi nzuri, inayokubali maji ya mvua, ikaotesha mimea mingi mibichi na mikavu, watu wakanufanika nayo. Wa pili: Ardhi inayotunza maji lakini haioteshi mimea, yenyewe inahifadhi maji ili watu wanufaike nayo; wanakunywa na kunywesha mifugo yao na mazao yao. Wa tatu: Ni Ardhi tambarare kavu haitunzi maji na wala haioteshi mazao, yenyewe haikunufaika na maji hayo, na wala watu hawakunufaika nayo. Ndivyo hivyo wenye kusikiliza yale aliyotumwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa elimu na uongofu. Wa kwanza: Ni mwanachuoni mwenye utambuzi katika dini, mwenye kuifanyia kazi elimu yake, mwenye kumfundisha mwingine; huyu yuko katika nafasi ya Ardhi nzuri, iliyokunywa ikanufaika yenyewe na ikaotesha ikamnufaisha mwingine. Wa pili: Ni yule aliyehifadhi elimu lakini hana uelewa na namna ya kuitumia, huyu kakusanya elimu, na amemaliza muda wake wote kwa hilo, isipokuwa yeye hajafanyia kazi sunna zake, na wala hana uelewa wa yale aliyoyakusanya; yeye ni mfano wa chombo kwa wengine, na yeye ni sawa na Ardhi ambayo maji hutuama ndani yake na watu wakanufaika nayo. Wa tatu: Ni yule anayesikia elimu lakini haihifadhi, na wala haifanyii kazi, na wala hainukuu kumpa mwingine; huyu ni kama Ardhi kavu ngumu isiyokuwa na mimea ndani yake, wala haikubali maji au inayomharibia mwingine.
Mafunzo
Kumebainishwa ubora wa kutafuta elimu na kuifundisha, na tahadhari ya kuipuuza.
Ni vizuri kupiga mifano ili kusogeza karibu maana iliyokusudiwa kwa watu.
Amesema Qurtubi: Kama ambavyo mvua huuhuisha mji uliokufa hivyo hivyo pia elimu ya dini huhuisha moyo uliokufa, kisha akawafananisha wenye kumsikiliza na Ardhi iliyotofauti inayoteremkiwa na maji.
Watu katika kuipokea elimu ya kisheria wako daraja tofauti tofauti.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 27) (79).
صحيح مسلم (4/ 1787) (2282).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 464).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 294).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 950).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia yeye tatizo katika matatizo ya siku ya Kiyama, na atakayemfanyia wepesi mwenye ugumu (katika jambo lake) Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi duniani na Akhera, na atakayemsitiri muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu humsaidia mja pale mja anapokuwa katika kumsaidia ndugu yake, na atakayeshika njia akitafuta ndani yake elimu, Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kupitia njia hiyo njia ya kuingia peponi, na hawajawahi kukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakisomeshana baina yao, isipokuwa huwashukia utulivu na huwagubika rehema na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwataja (vizuri) kwa wale walioko kwake (Malaika), na yeyote ambaye matendo yake yatamchelewesha kuingia peponi basi ukoo wake hautompeleka mbio (kuingia)".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa malipo ya muislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kulingana na yale anayoyatenda muislamu pamoja na waislamu wenzake; atakayetatua na akafariji na akaondoa, na ampa nafuu muumini ya dhiki na tabu miongoni mwa shida za dunia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa kumtatulia tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya Kiyama. Na atakayemfanyia wepesi mwenye hali ngumu na akamrahisishia na akamuondolea ugumu wake, basi naye Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi katika dunia na Akhera. Na atakayemsitiri muislamu, kama akiyaona kwake yale yasiyofaa kudhihirishwa katika mapungufu na kuteleza, basi naye Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anakuwa mwenye kumsaidia mja wake, pale ambapo mja anapokwenda mbio kumsaidia ndugu yake katika masilahi yake ya dunia na Akhera, na msaada unakuwa kwa kumuombea dua, au kwa mwili na mali na mengineyo. Na atakayekwenda kwa ajili kutafuta elimu ya kisheria, akikusudia kupata radhi za Mwenyezi Mugnu Mtukufu; Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kwa elimu hiyo njia ya kuingia pepnoni. Na hawatojikusanya watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu, wakikisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakifundishana baina yao, isipokuwa huwateremkia utulivu na amani, na huwafunika na kuwaenea rehema ya Mwenyezi Mungu, na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwasifia kwa wale walio karibu kwake, na inatosha kuwa ni fahari kwa mja kutajwa na Mwenyezi Mungu kwa wale walioko juu. Na yatakayekuwa matendo yake ni pungufu, hayatomuunganisha na watu wenye vyeo kwa ajili ya matendo yao, anatakiwa asibweteke kwa utukufu wa nasaba na ubora wa baba zake, na akafanya uzembe katika amali.
Mafunzo
Amesema bin Daqiiq Al-Idd: Hadithi hii ni tukufu mno, imekusanya aina mbali mbali za elimu na kanuni na adabu, ndani yake kuna fadhila za kukidhi haja za waislamu na kuwanufaisha kwa kadiri ya uwezo, kama elimu, au mali, au msaada, au kumuelekeza katika masilahi, na nasaha, au mengineyo.
Himizo la kumfanyia wepesi mwenye hali ngumu.
Himizo la kumsaidia mja muislamu, nakuwa Mwenyezi Mungu anamsaidia mwenye kusaidia kulingana na masada wake kwa ndugu yake.
Miongoni mwa kumsitiri muislamu: Ni kutochunguza aibu zake, na imepokelewa kutoka kwa mmoja kati ya wema waliotangulia alisema kuwa: Niliishi na watu hawakuwa na aibu, waliposema aibu za watu, na watu wakasema aibu zao, na niliishi na watu hawakuwa na aibu, wakajizuia kuzungumza aibu za watu, zikasahaulika aibu zao.
Si katika kuwasitiri watu kuacha uovu utendeke na kutoukemea, bali anaukemea na anasitiri, na hii ni kwa yule ambaye hajulikani kwa uovu na kuendelea katika ujeuri, na ama mwenye kufahamika kwa uovu, huyu hastahiki kusitiriwa, bali swala lake linafikishwa kwa mwenye mamlaka, kama hatohofia madhara kwa hilo; na hii ni kwa sababu kumsitiri kunamhadaa ili aendelee kuwaudhi watu, na anampa ujasiri mwingine katika watu wa shari na ukaidi.
Himizo la kutafuta elimu na kusoma Qur'ani na kujifunza.
Amesema Nawawi: Katika hili kuna dalili ya ubora wa kukusanyika katika kuisoma Qur'ani msikitini...na kunaunganishwa na msikiti katika fadhila hizi kukusanyika katika madrasa, na jihadi, na mfano wake, in shaa Allah.
Malipo Mwenyezi Mungu ameyaweka katika matendo na si katika ukoo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2074) (2699).
التحفة الربانية، لإسماعيل الأنصاري (ص82).
الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد، لعبد الله المحسن (ص69).
شرح الأربعين النووية ، لابن عثيمين (ص355).
عن معاوية رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ، وَإِنَّمَا أَنَا قَاسِمٌ، وَاللهُ يُعْطِي، وَلَنْ تَزَالَ هَذِهِ الْأُمَّةُ قَائِمَةً عَلَى أَمْرِ اللهِ، لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَالَفَهُمْ، حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ».
Imepokewa kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah humpa ufahamu katika dini, mimi ni mgawaji tu, na Allah ndiye anayetoa, na umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mwenye kutakiwa kheri na Mwenyezi Mungu basi humruzuku ufahamu katika dini yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mgawaji na msambazaji wa yale aliyopewa na Allah Mtukufu katika riziki na elimu na mengineyo, nakuwa mtoaji halisia ni Allah, na ama asiyekuwa yeye hao ni sababu tu hawawezi kunufaisha ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, nakuwa umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka Kiyama kisimame.
Mafunzo
Utukufu na fadhila za elimu ya kisheria na kujifunza kwake na kuihimiza.
Kuisimamia haki ni lazima kuwepo katika umma huu, likiwacha kusimamia kundi fulani linasimama kundi jingine.
Kuisoma dini ni katika matashi ya Allah Mtukufu kumtakia kheri mja wake.
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anatoa kwa amri ya Mwenyezi Mungu na matashi yake, na yeye hamiliki chochote.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 25) (71).
صحيح مسلم (2/ 718) (1037).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 485).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 324).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 424).
سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 688).
Kutoka kwa Abuu Umama Al-Baahili radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Walitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu wawili, mmoja wao mchamungu na mwingine msomi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ubora wa msomi kwa mchamungu, ni kama ubora wangu mimi kwa aliyechini yenu", Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake na wakazi wa mbinguni na ardhini hata mdudu chungu katika shimo lake na hata samaki humtakia rehema mwenye kuwafundisha watu mambo ya kheri".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo
Maelezo
Walitajwa watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mmoja wao ni mchamungu, na mwingine msomi, ni yupo mbora kati yao?
Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ubora wa msomi wa elimu ya kisheria mwenye kuifanyia kazi na mwenye kuifundisha kwa mchamungu aliyejitenga kwa ajili ya ibada, pamoja na kujua kwake yale ya wajibu kwake katika elimu ni kama ubora wake rehema na amani ziwe juu yake na utukufu wake kwa Swahaba wa chini zaidi. Kisha akabainisha rehema na amani ziwe juu yake sababu ya hilo, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika wake miongoni mwa wabeba Arshi, na wakazi wa mbinguni katika Malaika wengineo, na wakazi wa Ardhi kwanzia binadam na majini na wanyama wote, hata mdudu chungu katika makazi yake ndani ya tumbo la Ardhi, na hata nyangumi na samaki wa Baharini; alitaja hivi ili waingie katika kauli hii viumbe wa nchi kavu na Baharini, wote hawa wanamuombea mazuri mwenye kuwafundisha watu elimu ya dini ambayo ndani yake kuna uokovu wa watu na mafanikio yao.
Mafunzo
Miongoni mwa nyenzo za kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni kuhamasisha na kupiga mifano.
Ukubwa wa utukufu wa wanachuoni, wale waliojifunza elimu na wakatekeleza haki yake, kama kuifanyia kazi na kuifikisha.
Himizo la kuwaheshimu wanachuoni na wanafunzi, na kuwaombea dua.
Himizo la kwafundisha watu mambo ya kheri; kwa sababu ndio kufaulu kwao na furaha yao.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 416) (2685).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 481).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (1/ 298).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (4/ 432).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 469).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص758).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 954).
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kung'arisha na muonekano na uzuri katika dunia, na amfikishe Mwenyezi Mungu katika mng'ao wa peponi na neema zake na mng'ao wake katika Akhera; kwa yule atakayesikia hadithi yake akaihifadhi ili amfikishie mwingine, huenda aliyenukuliwa hadithi akawa mwerevu na muelewa na akawa na uwezo wa kuchambua hukumu kuliko hata aliyeinukuu hadithi, akawa wa kwanza anahifadhi vizuri, na wa pili akawa anauelewa na uchambuzi mzuri.
Mafunzo
Himizo la kuhifadhi mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuyafikisha kwa watu.
Kumebainishwa fadhila za watu wa hadithi, na heshima ya kuitafuta kwake.
Fadhila ya wanachuoni, ambao wanastahiki kuchambua na kuzielewa hadithi.
Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, wao ndio waliosikia hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakatufikishia.
Amesema Al-Munaawi: Amebainisha kuwa mpokezi wa hadithi kuwa na uelewa si katika sharti zake, bali sharti lake ni kuhifadhi, na kwa msomi kuelewa na kuzingatia.
Amesema bin Uyaina: Hakuna yeyote anayetafuta hadithi isipokuwa kuna mng'ao katika uso wake kwa hadithi hii.
Kuhifadhi kwa wasomi wa hadithi kuna aina mbili: Kuhifadhi kwa moyo na kifua, na kuhifadhi kwa kitabu na mwandiko, na aina zote mbili zinakusanywa na dua iliyoko katika hadithi.
Ufahamu wa watu unatofautiana, huenda mfikishiwa akawa muelewa zaidi kuliko aliyesikia, na huenda aliyebeba maarifa ya sheria akawa si muelewa.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 394) (2657).
سنن ابن ماجه (1/ 157) (232).
مسند أحمد (7/ 221) (4157).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 476).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 446).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (3/ 206).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 496).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 956).
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nitawahadithieni Hadithi nimeisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hadithi hiyo hatowahadithia yeyote asiyekuwa mimi: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika alama za kukaribia Kiyama ni kuondolewa elimu ya sheria na kuondolewa kwake itakuwa ni kwa kufa wanachuoni. Na matokeo yake utazidi na utaenea ujinga, na uzinifu utaenea na uchafu, na unywaji pombe utazidi na idadi ya wanaume itapungua na ya wanawake itazidi; Mpaka itafikia hatua mwanaume mmoja atabeba mambo yao na kusimamia maslahi yao.
Mafunzo
Kumewekwa wazi baadhi ya alama za Kiyama.
Kujua muda wa Kiyama ni katika mambo ya ghaibu (yasiyoonekana wala kujulikana) ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha.
Himizo juu ya kujifunza elimu ya kisheria kabla ya kukosekana kwake.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 37) (5231)، صحيح مسلم (4/ 2056) (2671)، فتح الباري لابن حجر (9/ 330)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (20/ 213).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com