Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi

عَنْ أَبِي مُوسَى رَضيَ اللهُ عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَثَلُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ مِنَ الهُدَى وَالعِلْمِ كَمَثَلِ الغَيْثِ الكَثِيرِ أَصَابَ أَرْضًا، فَكَانَ مِنْهَا نَقِيَّةٌ، قَبِلَتِ المَاءَ، فَأَنْبَتَتِ الكَلَأَ وَالعُشْبَ الكَثِيرَ، وَكَانَتْ مِنْهَا أَجَادِبُ، أَمْسَكَتِ المَاءَ، فَنَفَعَ اللَّهُ بِهَا النَّاسَ، فَشَرِبُوا وَسَقَوْا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَتْ مِنْهَا طَائِفَةً أُخْرَى، إِنَّمَا هِيَ قِيعَانٌ لاَ تُمْسِكُ مَاءً وَلاَ تُنْبِتُ كَلَأً، فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقُهَ فِي دِينِ اللَّهِ وَنَفَعَهُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ، فَعَلِمَ وَعَلَّمَ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأْسًا، وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللَّهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ».
Kutoka kwa Abuu Musa radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake, amesema: "Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi, kukawa na kundi moja zuri lililokubali maji likaotesha malisho na majani mengi, na ilikuwa ni ardhi ni kame iliyomeza maji Mwenyezi Mungu akanufaisha watu kupitia ardhi hiyo wakanywa na wakanywesha na wakalima, na mvua hiyo ikashuka katika sehemu nyingine ya ardhi laini haitulizi maji na wala haioteshi mimea; Huu ndio mfano wa mtu aliyejifunza akaelimika katika dini ya Mwenyezi Mungu na yakamnufaisha aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu akajua na akafundisha, na mfano mwingine ni wa mtu ambaye hakuyatilia maanani na wala hakukubali uongofu wa Mwenyezi Mungu ambao nimetumwa nao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amefananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kumstaajabu yule anayenufaika na yale aliyokuja nayo miongoni mwa muongozo na njia inayomfikisha mtu katika lengo, na elimu ya kisheria na Ardhi ambayo inashukiwa na mvua nyingi; ikawa migawanyiko mitatu: Wa kwanza: Ardhi safi nzuri, inayokubali maji ya mvua, ikaotesha mimea mingi mibichi na mikavu, watu wakanufanika nayo. Wa pili: Ardhi inayotunza maji lakini haioteshi mimea, yenyewe inahifadhi maji ili watu wanufaike nayo; wanakunywa na kunywesha mifugo yao na mazao yao. Wa tatu: Ni Ardhi tambarare kavu haitunzi maji na wala haioteshi mazao, yenyewe haikunufaika na maji hayo, na wala watu hawakunufaika nayo. Ndivyo hivyo wenye kusikiliza yale aliyotumwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa elimu na uongofu. Wa kwanza: Ni mwanachuoni mwenye utambuzi katika dini, mwenye kuifanyia kazi elimu yake, mwenye kumfundisha mwingine; huyu yuko katika nafasi ya Ardhi nzuri, iliyokunywa ikanufaika yenyewe na ikaotesha ikamnufaisha mwingine. Wa pili: Ni yule aliyehifadhi elimu lakini hana uelewa na namna ya kuitumia, huyu kakusanya elimu, na amemaliza muda wake wote kwa hilo, isipokuwa yeye hajafanyia kazi sunna zake, na wala hana uelewa wa yale aliyoyakusanya; yeye ni mfano wa chombo kwa wengine, na yeye ni sawa na Ardhi ambayo maji hutuama ndani yake na watu wakanufaika nayo. Wa tatu: Ni yule anayesikia elimu lakini haihifadhi, na wala haifanyii kazi, na wala hainukuu kumpa mwingine; huyu ni kama Ardhi kavu ngumu isiyokuwa na mimea ndani yake, wala haikubali maji au inayomharibia mwingine.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa ubora wa kutafuta elimu na kuifundisha, na tahadhari ya kuipuuza.
  2. Ni vizuri kupiga mifano ili kusogeza karibu maana iliyokusudiwa kwa watu.
  3. Amesema Qurtubi: Kama ambavyo mvua huuhuisha mji uliokufa hivyo hivyo pia elimu ya dini huhuisha moyo uliokufa, kisha akawafananisha wenye kumsikiliza na Ardhi iliyotofauti inayoteremkiwa na maji.
  4. Watu katika kuipokea elimu ya kisheria wako daraja tofauti tofauti.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 27) (79). صحيح مسلم (4/ 1787) (2282). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 464). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 294). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 950).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora wa Elimu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com

Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfano wa mvua kubwa iliyonyesha katika ardhi · Hadithi zenye maelezo · Sabīl