Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea.

عن أنس رضي الله عنه مرفوعاً: «من خَرج في طلب العلم فهو في سَبِيلِ الله حتى يرجع».
Kutoka kwa Anas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake hadithi Marfu'u: "Yeyote atakayetoka katika kutafuta elimu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka atakaporejea".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri
Maelezo

Maana ya hadithi: Nikuwa atakayetoka nyumbani kwake au katika mji wake; kwaajili ya kutafuta elimu ya kisheria,huyo anakuwa katika hukumu ya aliyetoka kwaajili ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,mpaka atakaporudi kwa watu wake; kwasababu anakuwa ni kama mpiganaji katika kuihuisha kwake dini na kumdhalilisha shetani na kuitaabisha nafsi.

Mafunzo
  1. Nikuwa kutafuta elimu ni kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu.
  2. Mwenye kutafuta elimu ana malipo ya mpiganaji katika viwanja vya mapambano; kwasababu wote hao wanayasimamia yale yanayoweza kuipa nguvu sheria ya Mwenyezi Mungu na wanazuia yasiyokuwa humo.
  3. Ndani yake nikuwa mwenye kutoka katika kutafuta elimu atakuwa na malipo ya kutembea kwake na kwenda kwake na kurudi kwake mpaka atakaporejea kwa watu wake.
Marejeo

جامع الترمذي، تحقيق وتعليق:أحمد محمد شاكر وآخرون، مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي، ط2، مصر، 1395هـ. دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، لمحمد علي بن محمد بن علان، ط4، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة، بيروت، 1425ه. رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ. رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ. صحيح الترغيب والترهيب، للألباني، ط5، مكتبة المعارف – الرياض. مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للمباركفوري، الطبعة الثالثة، إدارة البحوث العلمية والدعوة والإفتاء، الجامعة السلفية - بنارس الهند، 1404هـ. مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري، ط1، دار الفكر، بيروت، 1422هـ. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora wa Elimu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com