عَنْ زِيَادِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه قَالَ: ذَكَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا، فَقَالَ: «ذَاكَ عِنْدَ أَوَانِ ذَهَابِ الْعِلْمِ» قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَكَيْفَ يَذْهَبُ الْعِلْمُ، وَنَحْنُ نَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَنُقْرِئُهُ أَبْنَاءَنَا وَيُقْرِئُهُ أَبْنَاؤُنَا أَبْنَاءَهُمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ؟ قَالَ: «ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ زِيَادُ، إِنْ كُنْتُ لَأُرَاكَ مِنْ أَفْقَهِ رَجُلٍ بِالْمَدِينَةِ، أَوَلَيْسَ هَذِهِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى يَقْرَؤونَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنْجِيلَ، لَا يَعْمَلُونَ بِشَيْءٍ مِمَّا فِيهِمَا؟!».
Imepokelewa kutoka kwa Ziyaad Bin Labiid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu" Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni vipi inaondoka elimu, na hali yakuwa sisi tunaisoma Qur'ani na tunawasomesha watoto wetu na watoto wetu wanawasomesha watoto wao mpaka siku ya Kiyama? Akasema: "Akukose mama yako ewe Ziadi ikiwa nitakuzingatia wewe ni miongoni mwa wajuzi katika mji wa Madina, hivi hawa siyo Mayahudi na Manaswara wanaisoma Taurati na Injili, na hawafanyii kazi chochote katika yale yaliyomo?!"
Imepokelewa na Ibnu MaajahDarajaNi sahihi kwa sababu ya hadithi nyinginezo
Maelezo
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amekaa kati ya Maswahaba zake, akasema: Huu ndiyo wakati ambao itaondolewa na kupokonywa elimu kutoka kwa watu, Hivyo akashangaa Ziyaad Bin Labiid Al-Answaariy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Akasema: Ni vipi itaondolewa elimu na kutupotea sisi?! Na hali yakuwa tumeisoma Qur'ani na tukaihifadhi; Namuapia Mwenyezi Mungu kuwa tutaisoma, na kuwasomesha wake zetu na watoto wetu, na wajukuu wetu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa anaona ajabu: Amekukosa mama yako ewe Ziyaad! kama ikiwa nitakuzingatia wewe ni katika wajuzi wa mji wa Madina! Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akaweka wazi kuwa kuiokosa elimu siyo kuikosa Qur'ani, bali kukosa elimu ni kuacha kuifanyia kazi, Kwa mfano hii hapa Taurati na Injili ipo kwa Mayahudi na Manaswara; na pamoja na hivyo haiwanufaishi, wala hawapati faida kutokana na makusudio yake; na faida yenyewe ni kufanyia kazi walicho jifunza.
Mafunzo
- Kuwepo kwa Misahafu na vitabu kwenye mikono ya watu, haviwafai pasina kuvifanyia kazi.
- Kuondoshwa elimu kunakuwa kwa mambo mengi, miongoni mwayo ni: Kufariki kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kufa kwa Maulamaa, na kuacha kuifanyia kazi elimu.
- Miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondoka elimu na kuacha kuifanyia kazi.
- Kuhimizwa kuifanyia kazi elimu, na hayo ndiyo makusudio.
Marejeo
سنن ابن ماجه (5/ 172) (4048)، سنن الترمذي (4/ 328) (2653)، مسند أحمد (39/ 417) (23990)، الكاشف عن حقائق السُّنن (2/721)، المفهم (6/705)، مشارق الأنوار الوهاجة (2/146)، مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (24/ 274).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ لِتُبَاهُوا بِهِ الْعُلَمَاءَ، وَلَا لِتُمَارُوا بِهِ السُّفَهَاءَ، وَلَا تَخَيَّرُوا بِهِ الْمَجَالِسَ، فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ، فَالنَّارُ النَّارُ».
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu, wala kuonekana ni mtu bora kwenye vikao, na yeyote atakaye fanya hivyo basi anastahiki kuingia motoni."
Imepokelewa na Ibnu MaajahDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutafuta elimu kwa lengo la kujifaharisha kuwa naye ni katika Maulamaa, na kujitangaza kuwa mimi ni mjuzi kama nyinyi, au kwa ajili ya kujadiliana na wasiokuwa na ujuzi katika dini wenye upungufu wa maarifa, au anajifunza ili aonekane kuwa mtu bora kwenye vikao na kupewa kipaumbele kuliko mtu mwingine, Basi yeyote atakaye fanya hivyo; Bila shaka anastahiki kuchomwa katika moto kwa sababu ya kujionesha kwake na kukosa Ikhlaas katika kuitafuta elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Vitisho vikali vya kuingizwa motoni kwa mwenye kujifunza elimu ili ajifaharishe au ajadiliane kwa elimu yake au aonekane kuwa ni mtu bora kwenye vikao na mfano wa hayo.
- Umuhimu wa kuitakasa nia kwa kila mwenye kuitafuta elimu na kuifundisha.
- Nia ni msingi wa matendo, na kwa kupitia nia ndipo hupatikana malipo.
Marejeo
سنن ابن ماجه (1/ 170) (254)، مرشد ذوي الحجا والحاجة (2/378)، مشارق الأنوار الوهاجة ومطالع الأسرار البهاجة في شرح سنن الإمام ابن ماجه (4/ 482).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «إِذَا مَاتَ الْإِنْسَانُ انْقَطَعَ عَنْهُ عَمَلُهُ إِلَّا مِنْ ثَلَاثَةٍ: إِلَّا مِنْ صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ، أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amali za maiti hukatika kwa kufa kwake, hayapatikani mema tena baada ya kifo chake isipokuwa kwa mambo haya matatu; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya kupatikana kwake:
La kwanza: Sadaka yenye kuendelea thawabu zake na kudumu, isiyokatika, kama wakfu, na kujenga msikiti, na kuchimba visima, na mengineyo.
La pili: Elimu wanayonufaika nayo watu, kama kutunga vitabu vya kielimu, au kama kumfundisha mtu, yule naye akaisambaza elimu hiyo baada ya kifo chake.
La tatu: Mtoto mwema muumini wa kumuombea dua mzazi wake.
Mafunzo
- Wamekubaliana wanachuoni kuwa katika mambo yanayomfuata mwanadam baada ya kufa kwake katika thawabu ni: Sadaka ya kuendelea, na elimu yenye kunufaisha watu, na dua, na imekuja Hija katika hadithi zingine pia.
- Yametajwa mambo haya matatu pekee katika hadithi; kwa sababu ndio msingi wa mambo ya kheri, na ndio mambo wanayoyafanya watu wema wengi baada ya kuondoka kwao.
- Kila elimu yenye kunufaisha basi hupatikana malipo kwa elimu hiyo, lakini kilele chake ni elimu ya kisheria na elimu za msingi kwake.
- Elimu ndiyo yenye manufaa zaidi kati ya haya matatu; Kwa sababu elimu inamnufaisha mtu anayeisoma, elimu inahusisha kuihifadhi Sheria, inawanufaisha watu kwa ujumla, na ni pana zaidi na ni ya jumla, kwa sababu anajifunza kutoka katika elimu yako aliyepo wakati wa uhai wako na atakayekuwepo baada ya kufa kwako.
- Himizo la kulea watoto wema; Wao ndio wanaowanufaisha wazazi wao Akhera, na miongoni mwa manufaa yao ni kuwaombea dua.
- Himizo la kuwatendea wema wazazi wawili baada ya kufa kwako, nao ni katika wema ambao mtoto anafaidika nao.
- Dua inamnufaisha maiti hata kama haikutoka kwa mtoto, lakini katajwa mtoto pekee kwa sababu ndiye atakayeendelea kumuombea dua mtu mara nyingi mpaka kufa kwake.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1255) (1631)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (28/ 413).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com