Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 97

At-Tawba 9:97

التوبة

ٱلْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا۟ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Mabedui ndio wenye ukafiri mkubwa zaidi na unafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mabedui wamezidi sana katika ukafiri na unaafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. [97]

[97] Mabedui, Waarabu wa majangwani, ndio wakubwa wa kuikataa Haki na wa unaafiki. Hao hakika wamefika upeo wa mwisho katika hayo. Na hayo ni hivyo kwa kuwa wao wapo mbali na maarifa na mwahali mwenye vitovu vya ilimu. Na wao ndio wameelekea zaidi kuwa wasiijue mipaka ya Mwenyezi Mungu, na aliyo mteremshia Mtume wake katika sharia na hukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa pande zote mbili, na ni Mwenye hikima katika malipo anayo yakadiria.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mabedui, wakazi wa jangwani, ni washupavu zaidi wa ukafiri na unafiki kuliko wakazi wa mjini. Hivyo ni kwa sababu ya ugumu wa tabia zao, ususuavu wa nyoyo zao na kuwa mbali kwao na elimu, wanavyuoni, vikao vya mawaidha na dhikr (kumtaja Allah Mtukufu). Kwa hivyo wao wanastahili zaidi wasijue mipaka ya Dini na zile sheria na hukumu ambazo Allah Mtukufu Ameziteremsha. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa hali za hawa wote, Ni mwenye hekima katika uendeshaji Wake mambo ya waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net