At-Tawba
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
ٱلْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا۟ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ 97
{97} Yeye Mtukufu Anasema: "Mabedui," nao ni wakazi wa jangwani na nyikani, "ndio wenye ukafiri mkubwa zaidi na unafiki” kuliko wakazi wa mjini ambao wana ukafiri na unafiki ndani yao. Na hayo ni kwa ajili ya sababu nyingi. Miongoni mwake ni kwamba, wako mbali na elimu ya sheria za kidini, na matendo, na hukumu za kidini. Basi wao ndio wanaofailia zaidi “na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake” miongoni mwa misingi ya imani na hukumu za maamrisho mbalimbali na makatazo. Kinyume na wakazi wa mjini, wao wako karibu zaidi na kujua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake, na kwa sababu ya elimu hii wanakuwa na fikira nzuri na matashi ya heri ambayo wanaijua jambo ambalo halipo jangwani. Nao pia wana maumbile ya upole na kumfuata mlinganiaji, jambo ambalo haliko katika jangwa. Nao pia wanakaa pamoja na watu wa imani na kuchanganyika nao zaidi kuliko watu wa jangwani. Basi kwa sababu hiyo, ndiyo wakawa wanastahili zaidi kuwa na heri kuliko watu wa jangwani. Na ingawa kuna makafiri na wanafiki katika jangwa na katika miji, katika jangwa ni kali zaidi na kubwa zaidi kuliko katika miji.