Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 98

At-Tawba 9:98

التوبة

وَمِنَ ٱلْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَآئِرَةُ ٱلسَّوْءِ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Na katika Mabedui hao kuna yule anayefikiri kuwa kile anachotoa ni gharama ya bure, na anakutazamieni mambo yawageukie. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika Mabedui hao wapo wanao fikiri kuwa wanayo yatoa ni gharama ya bure, na wanakungojeleeni mambo yakugeukieni. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. [98]

[98] Na baadhi ya hawa wanaafiki katika watu wa majangwani wanaona kuwa wanacho kitoa katika Sabiili-Llahi (Njia ya Mwenyezi Mungu) kuwa ni gharama na khasara ya bure, kwa kuwa vile hawaamini kuwa kuna malipo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nao wanataraji na wanangojea hali ya vita ikugeukieni nyinyi Waumini. Bali hayo mageuko yatawageukia wao! Na hiyo shari wanayo ingojea ikufikieni itawafika wao iwazunguke! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzisikia kauli zao, na Mwenye kuvijua vitendo vyao na niya zao, na madhambi wanayo yachuma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miogoni mwa Mabedui kuna wanaohesabu wanachokitoa katika njia ya Allah Mtukufu kuwa ni kodi na ni hasara, hawatazamii, kwa kile wakitoacho, thawabu wala kujikinga na adhabu, na wana hamu mpatwe na misiba na maafa. Lakini mabaya yatawazunguka wao, sio Waislamu. Na Allah Mtukufu ni Msikizi wa wanayoyasema, ni Mjuzi wa nia zao mbaya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net