At-Tawba 9:99
التوبةوَمِنَ ٱلْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَـٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِ ۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِى رَحْمَتِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Na katika Mabedui kuna yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na anakichukulia kile anachotoa kuwa ni cha kumsongeza karibu na Mwenyezi Mungu na cha kupata kwacho dua za Mtume. Ndiyo! Hayo hakika ni mambo ya kuwasongeza karibu. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na katika Mabedui wapo wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaitakidi kuwa wanayo yatoa ndiyo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu na ya kuwapatia dua za Mtume. Naam! Hayo ni kweli mambo ya kuwasogeza. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mwenye kurehemu. [99]
[99] Wala si kama Mabedui wote ni hali hiyo. Wamo kati yao wanao muamini Mwenyezi Mungu, na wanaisadiki Siku ya Kiyama, na wanaitakidi kuwa kwa kutoa katika Njia ya Mwenyezi Mungu wanajikaribisha kwa Mwenyezi Mungu, na ni sababu ya Mtume s.a.w. kuwaombea wao, kwa kuwa yeye alikuwa akiwaombea kheri na baraka wale wanao toa sadaka. Na hayo bila ya shaka ni njia kubwa ya kuwakaribisha watu kwa Mwenyezi Mungu na kuwafikishia yale wayatakayo. Basi hakika Mwenyezi Mungu atawamiminia rehema yake, kwani Yeye ni Mwenye kusamehe madhambi, Mwenye kuwarehemu viumbe vyake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa Mabedui kuna wanaomuamini Allah Mtukufu na kukubali upweke Wake, kufufuliwa baada ya kufa na kuwa kuna thawabu na adhabu, na wanatarajia malipo mema kwa kile chochote wanachokitoa cha matumizi katika kupigana jihadi na washirikina, Kwa kukusudia radhi za Allah Mtukufu na mapenzi Yake, na kukifanya ni njia ya kumfanya apate maombi ya Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Jua utanabahi kwamba matendo haya yatawaweka wao karibu na Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Allah Mtukufu Atawatia kwenye Pepo Yake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha wa maovu waliyoyafanya, ni Mwenye kuwarehemu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net