Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 100

At-Tawba 9:100

التوبة

وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلْأَوَّلُونَ مِنَ ٱلْمُهَـٰجِرِينَ وَٱلْأَنصَارِ وَٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُم بِإِحْسَـٰنٍ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى تَحْتَهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Maana

Na wale waliotangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na wale waliowafuata kwa uzuri, Mwenyezi Mungu aliwaridhia, na wao walimridhia, na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. [100]

[100] Na Waumini walio tangulia kusilimu, na Wahajiri (walio hama Makka kwenda Madina) na Ansari (wasaidizi wa Madina walio wapokea) walio kwenda mwendo mzuri wala hawakufanya taksiri, Mwenyezi Mungu yu radhi nao. Basi anawapokea na anawalipa mema. Na wao kadhaalika wameridhika na wamefurahia aliyo waandalia Mwenyezi Mungu, nayo ni Mabustani yapitayo mito kati ya miti yake. Wataneemeka humo kwa neema ya milele. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale waliowatangulia watu mwanzo kwenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake miongoni mwa Muhajirûn waliowahama watu wao na jamaa zao wakaondoka kwenda kwenye Nyumba ya Uislamu, na Anṣãr waliomhami Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), dhidi ya maadui wake makafiri, na wale waliowafuata wao kwa wema, katika usawa wa itikadi, maneno na vitendo, kwa kutafuta radhi ya Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa pungufu na kutukuka, Hao ndio ambao Allah Mtukufu Ameridhika na wao kwa kumtii kwao Allah Mtukufu na Mtume Wake, na wao wameridhika na Yeye kwa malipo mazuri mengi Aliyowapatia kwa utiifu wao na Imani yao. Amewaandalia wao mabustani ya Pepo ambayo inapita mito chini yake, hali ya kukaa milele humo daima. Huko ndiko kufaulu kukubwa. Katika aya hii pana kuwasafisha Maswahaba, radhi za Allah Mtukufu ziwaendee, kuwafanya waadilifu na kuwasifu. Na kwa hivyo, kuwaheshimu wao ni katika misingi ya Imani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net