Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 101

At-Tawba 9:101

التوبة

وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ مُنَـٰفِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا۟ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ

Maana

Na katika mabedui walio jirani zenu kuna wanafiki; na katika wakazi wa Madina pia wapo wale waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa. [101]

[101] Na katika walio kuwa jirani na Madina miongoni mwa watu wa majangwani, walikuwako walio kuwa wakificha ukafiri wao na wakijidhihirisha kuwa ni Waumini. Na katika wakaazi wa Madina walikuwapo walio kuwa wamezoea unaafiki hata wakawa mabingwa, na wakawa wanauficha watu wasiutambue! Hata mwisho wewe, Mtume, usiwajue. Lakini Mwenyezi Mungu anajua hakika yao, na atawaadhibu duniani mara mbili - mara ya kwanza kwa kuwashinda maadui zenu, na hayo yatawaudhi wao; na mara nyingine kwa kuwafedhehi na kuwakashifu unaafiki wao. Tena, basi, watarejeshwa Siku ya Akhera kwenye adhabu ya Moto, na vitisho vyake vikubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Miongoni mwa watu ambao wako pembezoni mwa Madina kuna Mabedui wanafiki, na miongoni mwa watu wa Madina pia kuna wanafiki waliojikita kwenye unafiki na kuzidi kuendelea nao kwa kupita mipaka katika uasi, kwa namna ambayo yanafichamana kwako, ewe Mtume, mambo yao. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kwa kuuawa na kutekwa na kukashifiwa duniani, na kwa adhabu ya kaburi baada ya kufa, kisha watapelekwa, Siku ya Kiyama, kwenye adhabu kubwa ndani ya Moto wa Jahanamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net