Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 102

At-Tawba 9:102

التوبة

وَءَاخَرُونَ ٱعْتَرَفُوا۟ بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا۟ عَمَلًا صَـٰلِحًا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na wengine walikiri dhambi zao, walichanganya matendo mema na mengine mabaya. Huenda Mwenyezi Mungu akakubali toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wengine walikiri dhambi zao, wakachanganya vitendo vyema na vingine viovu. Asaa Mwenyezi Mungu akapokea toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [102]

[102] Na wapo watu wengine walio kuudhini, kisha baadae wakakubali makosa yao, na wakafuata Njia ya Haki. Basi watu hao wamefanya vitendo vyema na vitendo viovu. Kwa hao inatarajiwa kukubaliwa toba yao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemu waja wake; huikubali toba yao na huwasamehe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wengine wa Madina na walio pembezoni mwake, walikubali makosa yao, wakajuta na wakatubia kwa hayo, walichanganya matendo mazuri, nayo ni kutubia, kujuta, kukubali makosa na mengineyo miongoni mwa matendo mema, kwa mengine mabaya, nayo ni kujikalia nyuma kumuacha Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na mengineyo miongoni mwa matendo mabaya. Basi hao yatarajiwa Allah Mtukufu Awaelekeze kutubia na aikubali toba yao kutoka kwao. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye kuwarehemu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net