At-Tawba 9:103
التوبةخُذْ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwayo, na waombee dua. Hakika kuomba dua kwako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. [103]
[103] Ewe Mtume! Pokea kwa hawa wenye kutubu sadaka zao, uwasafishe kwa hizo sadaka makosa yao na uchoyo wao, na unyanyue daraja zao mbele ya Mwenyezi Mungu. Na waombee kheri na uwongofu; kwani kuomba kwako kutawapoza nafsi zao, na zitatulia nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maombi, Mwenye kuwajua wenye nyoyo safi katika toba zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Chukua, ewe Mtume, kwenye mali za hawa waliotubia, waliochanganya matendo mema na matendo mengine maovu, sadaka itakayowasafisha wao na uchafu wa madhambi yao na itakayowainua wao na kuwaondoa kwenye daraja za wanafiki kuwapeleka kwenye daraja za wenye ikhlasi; na watakie wao msamaha wa madhambi yao na uwaombee sitara ya hayo, kwani maombi yako na utakaji msamaha wako ni rehema na utulivu kwao. Na Allah Mtukufu ni Msikizi wa kila maombi na kila neno, ni Mjuzi wa hali za waja Wake na nia zao, na Atamlipa kila mwenye kutenda kwa matendo aliyoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net