At-Tawba 9:104
التوبةأَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقْبَلُ ٱلتَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِۦ وَيَأْخُذُ ٱلصَّدَقَـٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Je, hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anakubali toba ya waja wake, na anazichukua sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu sana?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anapokea toba ya waja wake, na anazikubali sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba na Mwenye kurehemu?. [104]
[104] Hebu na wajue hao wanao tubu kuwa hakika Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anaye kubali toba ya kweli, na sadaka iliyo safi, na kwamba Yeye Subhanahu ndiye Mkunjufu wa fadhila katika kukubali toba, Mkuu katika kuwarehemu waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hawajui, hawa wenye kujikalisha nyuma na kuacha kwenda kwenye jihadi na wengineo, kwamba Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Ambaye Anakubali toba ya waja Wake, Anachukua sadaka na Anatoa malipo yake, na kwamba Allah Mtukufu ni Mwingi wa kukubali toba ya waja Wake warejeapo Kwake, ni Mwenye kuwarehemu warudipo kutaka radhi Zake.?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net