Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 105

At-Tawba 9:105

التوبة

وَقُلِ ٱعْمَلُوا۟ فَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُۥ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَـٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Na sema: Tendeni matendo. Na Mwenyezi Mungu atayaona matendo yenu, na Mtume wake, na Waumini. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; basi naye atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda. [105]

[105] Ewe Mtume! Waambie watu: Tendeni wala msifanye taksiri katika vitendo vya kheri na kutekeleza waajibu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu vyote. Na Mtume na Waumini nao pia wataviona na watavipima kwa vipimo vya Imani, na wataviona kwa mujibu wa itakikanavyo. Kisha mtarudishwa baada ya kufa kwa Mwenye kuijua siri yenu na dhaahiri yenu, apate kukulipeni kwa vitendo vyenu, baada ya kukwambieni dogo lake na kubwa lake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na sema, ewe Nabii, kuwaambia hawa wenye kujikalisha nyuma na kuacha kwenda kwenye jihadi, «Mfanyieni Mwenyezai Mungu yale ya kumridhisha ya kumtii na kutekeleza mambo ya lazima Aliyoyaweka na kuepuka maasia. Na Allah Mtukufu Atayaona matendo yenu na Mtume Wake na Waumini, na yatakuwa wazi mambo yenu, na mtarejeshwa Siku ya Kiyama kwa Anayejua yaliyofichika yenu na yaliyo wazi yenu, na hapo Atawapa habari ya yale ambayo mlikuwa mkiyafanya. Katika hii kuna onyo kwa anayeendelea kwenye ubatilifu wake na ukiukaji mipaka wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net