Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 106

At-Tawba 9:106

التوبة

وَءَاخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Na wapo wengine wanaongojea amri ya Mwenyezi Mungu. Ima atawaadhibu au atawakubalia toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wapo wengine wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu - ama atawaadhibu au atawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. [106]

[106] Na wapo watu wengine wametumbukia katika madhambi - wameacha kwenda kwenye Jihadi, lakini hawana unaafiki. Watu hawa wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu. Ama awaadhibu au awakubalie toba yao awasamehe. Na Mwenyezi Mungu anazijua hali zao, na yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Naye ni Mwenye hikima kwa ayafanyayo kwa waja wake, ikiwa kuwalipa thawabu au adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa hawa waliojikalisha nyuma wakaacha kuwafuata, enyi Waumini, katika vita vya Tabûk kuna wengine walioahirishwa, ili Allah Mtukufu Aaamue juu yao uamuzi Atakaoutoa: ima Awaadhibu Allah Mtukufu au Awasamehe. Hawa ni wale waliojuta kwa yale ambayo walifanya. Nao ni Murãrah mwana wa al-Rabî‘, Ka‘b mtoto wa Mãlik na Hilãl mtoto wa Umayyah. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa Anayestahili mateso au msamaha. Ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake yote na vitendo Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net