At-Tawba 9:107
التوبةوَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًۢا بَيْنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَآ إِلَّا ٱلْحُسْنَىٰ ۖ وَٱللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ
Na wapo waliojenga msikiti kwa ajili ya madhara, na ukafiri, na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa ajili ya wale waliompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: 'Hatukukusudia isipokuwa uzuri tu.' Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao hakika ni waongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wapo walio jenga msikiti kwa ajili ya madhara na ukafiri na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa walio mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: Hatukukusudia ila wema tu. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo. [107]
[107] Na miongoni mwa wanaafiki walikuwapo jamaa walio jenga msikiti si kwa kutafuta ridhaa ya Mwenyezi Mungu, bali wakikusudia madhara, na kufuru, na kuwagawa Waumini. Na wao wataapa kuwa wao hawakutaka kwa kujenga msikiti huo ila kheri na a'mali njema. Na Mwenyezi Mungu anawashuhudia kuwa ni waongo katika hiyo Imani yao. Msikiti ulio tajwa katika Aya ulijengwa na baadhi ya wanaafiki wa Madina walio azimia shari. Waliudhika kujengwa Masjid Qubaa walio ujenga Banu Amri bin Auf, na akaubariki Mtume s.a.w. kwa kuswali ndani yake. Basi Ibn Aamir Arrahib (aliye itwa Rahib, Mmonaki, kwa kushirikiana kwake na Mapadri) aliwachochea hao wanaafiki wajenge nao Msikiti wa ushinde kushindana na walio jenga Masjid Qubaa, ili uwepo ushinde wa kijahili kwa kila mmoja kujitapa kwa kujenga msikiti. Vile vile ilikuwa azma yao wafanye hapo ni kioteo pa kukutania siri kupanga njama za kuwadhuru Waumini. Baada ya kwisha jenga walimualika Mtume s.a.w. ende kuswali humo, wafanye hiyo sala ndio ada tena ya ushindani wao na kuwafarikisha Waumini. Mtume alitaka kuitikia wito wao bila ya kujua njama zao. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjuvya alipo kuwa anarudi kutoka vita vya Tabuk na azma yake ya kuitikia wito. Na Yeye Subhanahu akamkataza asisimame kabisa katika msikiti huo, licha ya kuswali ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanafiki waliojenga msikiti, kwa kuwadhuru Waumini, kumkanusha Allah Mtukufu na kuwagawanya Waumini, ili waswali humo baadhi yao na wauache msikiti wa Qubã’ ambao Waislamu wanaswali ndani yake, ili Waislamu watafautiane na wagawanyike kwa hilo, na kwa ajili ya kumngojea yule aliyempiga vita Allah Mtukufu na Mtume Wake kabla ya hapo, naye ni Abû ‘Ãmir al Rãhib aliyeasi, ili pawe ni mahali pa kuwafanyia vitimbi Waislamu. Na wataapa tena wataapa, wanafiki hawa, kwamba wao hawakukusudia kwa kuujenga isipokuwa kuwafanyia wema na kuwahurumia Waislamu na kuwapa nafasi wanyonge wasioweza kwenda msikiti wa Qubã’ .Na Allah Mtukufu Anashuhudia kwamba wao ni warongo katika yale wanayoyaapia. Msikiti huo ulivunjwa na ukatiwa moto.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net