At-Tawba 9:108
التوبةلَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا۟ ۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُطَّهِّرِينَ
Usisimame ndani yake kabisa. Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa ucha Mungu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo wanaume wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Usisimame kwenye msikiti huo kabisa. Msikiti ulio jengwa juu ya msingi wa uchamngu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo watu wanao penda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao jitakasa. [108]
[108] Ewe Mtume! Usisali kabisa katika msikiti huo. Msikiti unao faa kupata rehema za Mwenyezi Mungu na radhi zake tangu mwanzo kama Masjid Qubaa ndio unao stahiki kusimamishwa ndani yake ibada za Mwenyezi Mungu. Katika msikiti huo wamo watu wanao penda kujinadhifisha miili yao na nyoyo zao kwa kutekeleza ibada zilizo sawa. Na Mwenyezi anawapenda na anawalipa thawabu wanao jikaribisha kwake kwa kujit'ahirisha nje na ndani, kiwiliwili na kiroho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Usisimame, ewe Nabii, kuswali katika msikiti huo kabisa. Kwani msikiti uliojengwa kwa misingi ya uchamungu kuanzia siku ya mwanzo, nao ni msikiti wa Qubã’, unafaa zaidi kwa wewe kusimama humo kwa kuswali. Kwani katika msikiti huu kuna watu wanapenda kujisafisha na najisi na uchafu kwa maji, kama wanavyojisafisha kwa kujiepusha na mambo yanayopelekea kufanya mambo yaliyoharamishwa na kuomba msamaha kutokana na madhambi na maasia. Na Allah Mtukufu Anawapenda wenye kujisafisha.Na iwapo msikiti wa Qubã’ ulijengwa juu ya misingi ya uchaji Mungu, basi Msikiti wa Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ni kama hivyo kwa njia ya ubora zaidi na ustahiki zaidi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net