At-Tawba 9:109
التوبةأَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَـٰنَهُۥ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَـٰنَهُۥ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَٱنْهَارَ بِهِۦ فِى نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Je, mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya uchaji utokao kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora zaidi au mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka? Kwa hivyo ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalo burugunyika, na likaburugunyika naye katika Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. [109]
[109] Hawi sawa katika itikadi yake wala katika vitendo vyake mwenye kusimamisha jengo lake kwa usafi wa niya katika kumcha Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, na yule mwenye kusimamisha jengo lake juu ya unaafiki, na ukafiri. Kwani vitendo vya mchamngu vimenyooka, vimejengeka juu ya msingi madhbuti. Na vitendo vya mnaafiki ni kama jengo lililo jengwa juu ya ukingo wa shimo. Jengo hilo litaporomoka tu, na litamtupa mwenyewe katika Moto wa Jahannamu. Na Mwenyezi Mungu hamuongoi kwenye Njia ya Uwongofu anaye shikilia kujidhulumu nafsi yake kwa ukafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawalingani: yule aliyeweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Allah Mtukufu na kumtii na kutaka radhi Zake na yule aliyeweka msingi wa jengo lake kandokando ya shimo linalokaribia kuanguka akajenga msikiti wa kudhuru, kukufuru na kuleta mgawanyiko baina ya Waislamu, ikampelekea yeye aanguke kwenye Moto wa Jahanamu. Na Allah Mtukufu Hawaongozi watu madhalimu waliokiuka mipaka Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net