Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 110

At-Tawba 9:110

التوبة

لَا يَزَالُ بُنْيَـٰنُهُمُ ٱلَّذِى بَنَوْا۟ رِيبَةً فِى قُلُوبِهِمْ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Na mjengo wao huo walioujenga hautaacha kuwa shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na jengo lao hilo walilo lijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. [110]

[110] Na hilo jengo lao walilo lijenga wanaafiki litakuwa ni sababu ya kuwakereketa na kuwatia khofu katika nyoyo zao. Hayeshi hayo mpaka zipasuke nyoyo zao kwa majuto na kutubu au wafe! Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, na Mwenye hikima katika vitendo vyake na malipo yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haliachi kuendelea, lile jengo wanafiki walilolijenga liwe ni madhara kwa msikiti wa Qubã’, kuwa ni ishara ya shaka na unafiki uliojikita ndani ya nyoyo zao, mpaka nyoyo zao zikatike katike kwa wao kuuawa au kufa au kwa kujuta kwao upeo wa kujuta na kurejea kwao kwa Mola wao na kumuogopa Yeye upeo wa kuogopa.Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa shaka waliyonayo hawa wanafiki na yale waliyoyakusudia kwa jengo lao, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo ya viumbe Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net