Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 111

At-Tawba 9:111

التوبة

إِنَّ ٱللَّهَ ٱشْتَرَىٰ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَٰلَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلْجَنَّةَ ۚ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِى ٱلتَّوْرَىٰةِ وَٱلْإِنجِيلِ وَٱلْقُرْءَانِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِۦ مِنَ ٱللَّهِ ۚ فَٱسْتَبْشِرُوا۟ بِبَيْعِكُمُ ٱلَّذِى بَايَعْتُم بِهِۦ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu alinunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao wana Bustani ya mbinguni. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha (Mwenyezi Mungu) kwa haki katika Taurati, na Injili, na Qur-ani. Na nani atimizaye zaidi ahadi yake zaidi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,. [111]

[111] Mwenyezi Mungu anatilia mkazo ahadi yake aliyo wapa Waumini wanao toa nafsi zao na mali yao kwa ajili ya Njia yake, kuwa hakika Yeye amenunua kwao hizo nafsi zao na mali yao kwa kuwalipa Pepo kuwa ndio thamani ya hivyo walivyo toa. Kwani wao wanapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Wanawauwa maadui wa Mwenyezi Mungu, au wao wanakufa mashahidi katika Njia yake. Na Mwenyezi Mungu amethibitisha ukweli huu katika Taurati na Injili, kama alivyo thibitisha katika Qur'ani. Wala hapana yeyote mwenye kumshinda Mwenyezi Mungu katika kutimiza ahadi. Basi furahini, enyi Waumini Mujaahidina, kwa biashara hii mlio uza nafsi zenu na mali yenu ambayo yatatoweka, na badala yake mkanunua Pepo itakayo baki milele. Na biashara hii ndio ushindi mkubwa kwenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Amenunua kutoka kwa Waumini, nafsi zao na kuwapa wao, badala yake, Pepo na yale Aliyoyatayarisha ya starehe humo ndani, kwa kutoa kwao nafsi zao na mali zao katika kupigana jihadi na maadui wake kwa ajili ya kulitukuza neno Lake na kuidhihirisha dini Yake, wakaua na wakauawa. Hiyo ikiwa ni ahadi juu ya Allah Mtukufu iliyothibiti ndani ya Taurati iliyoteremshwa kwa Mûsã, (amani imshukie), na Injili iliyoteremshwa kwa ‘Ǐsâ, (amani imshukie), na Qur’ani iliyoteremshwa kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani imshukie). Na hakuna yoyote mwenye utekelezaji zaidi wa ahadi Yake kuliko Allah Mtukufu, kwa yule aliyetimiza ahadi yake kwa Allah Mtukufu. Basi onesheni furaha, enyi Waumini, kwa biashara yenu mliyoifanya na Allah Mtukufu na kwa ahadi Yake, ya Pepo na Radhi, kwenu. Na mapatano hayo ya biashara ndiyo kufaulu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net