Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 112

At-Tawba 9:112

التوبة

ٱلتَّـٰٓئِبُونَ ٱلْعَـٰبِدُونَ ٱلْحَـٰمِدُونَ ٱلسَّـٰٓئِحُونَ ٱلرَّٰكِعُونَ ٱلسَّـٰجِدُونَ ٱلْـَٔامِرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَٱلنَّاهُونَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَٱلْحَـٰفِظُونَ لِحُدُودِ ٱللَّهِ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Wale wanaotubia, wanaoabudu, wanaohimidi, wanaokimbilia heri, wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu, na wanaolinda mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na wabashirie Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Kwa) wanao tubia, wanao abudu, wanao himidi, wanao kimbilia kheri, wanao rukuu, wanao sujudu, wanao amrisha mema na wanao kataza maovu, na wanao linda mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na wabashirie Waumini. [112]

[112] Sifa za wale walio uza nafsi zao kwa ajili ya Pepo ni kuwa wanakithirisha toba kwa Mwenyezi Mungu kwa kujikwaa kwao, na wanamhimidi katika kila hali, na wanakimbilia kwenda kujifanyia kheri nafsi zao na kuwafanyia wenginewe, na wanahifadhi Swala zao, na wanazitimiza kwa ukamilifu na unyenyekevu, na wanaamrisha kila kheri inayo wafikiana na Sharia ya Mwenyezi Mungu, na wanakataza kila uovu unao zuiliwa na Dini, na wanaishika Sharia ya Mwenyezi Mungu. Ewe Mtume! Wabashirie kheri Waumini!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa sifa za Waumini hawa waliopewa bishara njema ya kuingia Peponi ni kwamba wao ndio wanaotubia, wenye kuondoka kwenye yale ambayo Allah Mtukufu Ameyakataza kwenda kwenye yale ambayo Allah Mtukufu Anayapenda na Anayaridhia, wale waliomtakasia ibada Allah Mtukufu Peke Yake na wakapindana katika kumtii, wale wenye kumshukuru Allah Mtukufu kwa yote yale ambayo Aliwatahini nayo ya uzuri au ubaya, wenye kufunga, wenye kurukuu katika swala zao, wenye kusujudu katika hizo, wale ambao wanawaamrisha watu kila lile ambalo Allah Mtukufu na Mtume Wake wameliamrisha na wanawakataza kila lile ambalo Allah Mtukufu na Mtume Wake wamelikataza, wenye kutekeleza faradhi za Allah Mtukufu, wenye kumalizikia kwenye kufuata amri Yake na kuepuka katazo Lake, wenye kusimama imara katika kumtii na wenye kukomea pale penye mipaka Yake. Na wape bishara njema, ewe Nabii, waumini hawa waliosifika na sifa hizi ya radhi za Allah Mtukufu na Pepo Yake

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net