At-Tawba 9:113
التوبةمَا كَانَ لِلنَّبِىِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن يَسْتَغْفِرُوا۟ لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوٓا۟ أُو۟لِى قُرْبَىٰ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَحِيمِ
Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina, hata wakiwa ni jamaa zao, baada ya kwishawabainikia kuwa hao ni watu wa Motoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni. [113]
[113] Haimfalii Nabii na Waumini kuwatakia maghfira washirikina, hata ikiwa ni jamaa zao wa karibu kabisa, baada ya kwisha hao Waumini kuwajua kwamba hao washirikina wamekufa katika ukafiri. Kwani hao wamestahiki kukaa milele Motoni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haifai kwa Nabii Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina, hata kama ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwa imefunuka waziwazi kwamba wao ni watu wa Moto wa Jahîm, kwa kufa kwao katika hali ya ushirikina. Na Allah Mtukufu Hawasamehi washirikina, kama alivyosema Aliyetukuka, «Hakika Allah Mtukufu Hasamehi Ashirikishwapo» na kama Alivyosema Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, «Hakika yule anayemshirikisha Allah Mtukufu, basi Allah Mtukufu Ashamharimishia Pepo»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net